BOSI wa klabu ya
Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa nakuweka imani kuwa uongozi wa Liverpool ulikuwa
sahihi kutochukua hatua dhidi ya mshambuliaji wao Luis Suarez kabla ya
kufungiwa mechi 10 na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kumng’ata beki
wa Chelsea Branislav Ivanovic. Ferguson
amesema tukio hilo linamkumbusha jinsi walivyotendwa na FA baada ya
mshambuliaji wake Eric Cantona kumpiga teke la kung-fu mshabiki wa
Crystal Palace mwaka 1995. Ferguson
amedai kuwa FA iliwahakikishia kuwa hatachukua hatua zaidi kama United
watamuadhibu mchezaji huyo lakini pamoja na United kumfungia Cantona
miezi minne, chama hicho kiliongeza adhabu na kufikia miezi nane. Kwa matokeo hayo yaliyowakuta United kipindi hicho Ferguson amesema ameelewa kwanini Liverpool hawakumuadhibu nyota huyo mapema.