Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya unapenda kuwaarifu mashabiki na wadau wa Timu ya Mbeya City Fc kuwa suala lililojitokeza wiki iliyopita kuhusiana na kocha mkuu wa timu hii Juma Mwambusi kujiuzulu, litatolewa maelezo na ufafanuzi wiki ijayo.
Hivyo basi mashabiki na wadau wa timu ya Mbeya City Fc mnaombwa kutulia mpaka ufafanuzi au taarifa rasmi juu ya jambo hili itakapotolewa, pia mashabiki mnaombwa kuwa makini na baadhi ya watu ambao wanataka kutumia mwanya huu kuzusha chokochoko nyingi kwa lengo la kuleta mgawanyiko na kuvuruga umoja wetu.
Kwa sasa Juma Mwambusi bado ni mwalimu wa Mbeya City Football Club{Vikao vya ndani vinaendelea kuhusu suala hili}.