Friday, November 21, 2014

NDANDA YAJIWEKA FITI LIGI KUU YAJIPANGA KUSAJILI WA NGUVU.

Timu ya Ndanda FC katika kuhakikisha inatoa dozi Ligi Kuu Bara ya imeamua kusajili wachezaji kutoka Burundi na katika timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa ligi kuu, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar Heroes.

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji, Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Djibouti.

Selemani Kachele Katibu wa Ndanda, akizunghumza na mtandao huu amesema kuwa nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha dogo.

Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani katika msimamo wa ligi kuu  ikiwa na point 6, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar Heroes.

Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji, Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Djibouti.

Katibu wa Ndanda, Selemani Kachele amesema nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha dogo.