Saturday, June 22, 2013

MASAU BWIRE ASEMA TUPO VIZURI MSIMU UJAO WA VPL


Timu ya soka Ruvu Shooting Maafande wa kibaha mkoani pwani chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa “Masta” wamendelea kutangaza vita kwa klabu za ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, hususani Simba, Yanga na Azam fc.
Afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire akizungumza na mkali wa dimba amesema kuwa msimu ujao wa ligi kuu hakuna kulala, watapambana kufa na kupona kuhakikisha wanapata nafasi tatu za juu.
Masau amesema katika kuhakikisha wanafanikisha doto zao wameendelea kufanya vizuri katika usajili na mpaka sasa wamepata nyota watano.
Mchezaji  Juma Seif Dion "Kijiko" aliyekuwa akiichezea Africon Lyon msimu uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara naye amejiunga na Ruvu Shooting ya Pwani kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijiko aliyewahi pia kukipiga Yanga, alisaini mkataba huo  hivi karibuni katika ofisi za timu hiyo Mlandizi, Kibaha tayari kuitumikia kwa msimu ujao.
Kijiko ni mchezaji wa tano kusaini mkataba na timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi, wengine waliosaini ni Ciosmas Ader (Azam), Elias Maguli (Prison), Juma Nade (Kagera Sugar) na Lambale Jerome (Ashanti).
Wakati huo huo, uongozi wa timu hiyo ya Ruvu Shooting umetangaza kuwaacha wachezaji watano kutokana na kiwango chao cha kucheza mpira kushuka.
Aidha Masau Bwire amewataja wachezaji hao kua ni Pail Ndauka, Charles Nobart, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus Manyasi.
Kwa mujibu wa Bwire, timu hiyo tayari iko kambini kikosi cha Jeshi 832 Ruvu JKT, itaanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu, Juni 24 chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa.
Bwire amewataka wachezaji wote ambao kawajaripoti kambini wafike haraka kabla ya Jumatatu ikiwa ni pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.