Shirikisho la Soka Duniani FIFA leo limetangaza Listi ya Ubora Duniani kwa Nchi Wanachama na Mabingwa wa Dunia, Spain, wamebakiNambari
Wani na Tanzania pia kubaki Nafasi yao ile ile ya 122 huku Wenyeji wa
Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Juni 12, Brazil, wakipanda Nafasi 2
na kushika Nafasi ya 4.
Kukosekana kwa Mechi nyingi za Kimataifa
zinazotambuliwa na FIFA, zikichezwa 13 tu, kumefanya Listi hii mpya
isiwe na mabadiliko makubwa na Nchi 143 kubakia Nafasi zao zilezile za
Mwezi uliopita.
TANZANIA-Walipo na Nchi zilizo karibu yao:
122 Malawi {Chini 1}
122 Tanzania {Palepale}
124 Guatemala {Palepale}
125 Burundi {Palepale}
Nchi ya Afrika ambayo iko juu sana ni
Ivory Coast ambao wako Nafasi ya 21 ambayo pia waliishika Mwezi uliopita
na inayofuata ni Egypt walio Nafasi ya 24 kama Mwezi Aprili.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa Juni 5.
20 BORA:
[Kwenye Mabano Mabadiliko toka Listi ya Aprili]
1 Spain [Wamebaki walipo]
2 Germany [Palepale]
3 Portugal [Palepale]
4 Brazil [Juu Nafasi2]
6 Uruguay [Chini 1]
7 Argentina [Chini 1]
8 Switzerland [Palepale]
9 Italy [Palepale]
10 Greece [Palepale]
11 England [Palepale]
12 Belgium [Palepale]
13 Chile [Juu Nafasi 1]
14 USA [Chini Nafasi 2]
15 Netherlands [Palepale]
16 France [Palepale]
17 Ukraine [Palepale]
18 Russia [Palepale]
19 Mexico[Palepale]
20 Croatia [Palepale]