Timu ya
vijana chini ya umri wa miaka 20,Ngorongoro Heroes jioni hii imeambulia kipigo
cha mabao 2-0 dhidi ya Nigeria uwanja wa taifa jijini dare s salaam katika
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wa 20 ambapo
kwa matokeo hayo yamempa kazi ngumu kocha mkuu John Simkoko kusonga mbele.
Ngorongora
walipata nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha kwanza, lakini bado ugonjwa wa
kutotumia nafasi muhimu unazidi kuitafuna timu hii
Mshambuliaji
Saady Kipanga alishindwa kuonesha makeke yake baada ya kupoteza nafasi kadhaa
za kufunga.
Mpaka
dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika milango ya timu zote ilikuwa
migumu, huku kipa namba moja wa Heroes, Aishi Manula akiumia.
Kipindi
cha pili, Manula alishindwa kurejea uwanjani na kumpisha kipa namba mbili,
Peter Manyika.
Katika
Kipindi hicho cha pili Ngorongoro waliingia kizembe na kujikuta wakifungwa
mabao mawili na kumaliza mechi kwa kipigo cha nyumbani cha mabao mawili kwa
sifuri.