Wakala wa beki mahiri wa club ya Liverpool, Daniel Agger amesema kuwa Liverpool imeitupilia mbali ofa iliyotumwa
na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo. Barcelona imekuwa
ikihusishwa na kutaka kusajili mabeki kadhaa wa Ligi Kuu nchini
Uingereza ambapo tayari walishatoa kitita cha euro milioni 25 kwa ajili
ya beki wa Chelsea David Luiz. Chelsea waliweka wazi kuwa mabingwa wa
soka nchini Hispania wanapoteza muda wao na sasa wakala wa Agger aitwaye
Per Steffensen naye amebainisha kuwa Liverpool tayari wamepiga chini
ofa hiyo. Wakala huyo amesema mteja wake bado ana mkataba wa miaka
mitatu na Liverpool hivyo ni juu ya makubaliano ya klabu hizo mbili
kuhusu ada ya uhamisho.