Maximo alichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van Der Pluijm
huku Phiri akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba baada ya
kuchukua mikoba iliyoachwa na
Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyetimuliwa Jumapili iliyopita.
Katikamkutano na waandishi wa habari, Maximo amesema kuwa
amemkaribisha kocha huyo ambaye anafahamu kuwa ni mzuri lakini amemtaka
kutambua ushindani uliopo wa ligi ya Tanzania.
Maximo amesema napenda kumwambia kocha mpya wa Simba (Patrick
Phiri), karibu Tanzania lakini
ajue kuwa ligi ina ushindani wa hali ya juu japo natambua kuwa yeye ni kocha
mzuri na anayeifahamu ligi ya hapa”, alisema Maximo.
Phiri ametua nchini siku chache zilizopita na kusaini
mkataba wa mwaka
mmoja kuinoa Simba, hii ikiwa ni mara ya tatu tofauti kuionoa
timu hiyo.
Kwa upande mwingine, Maximo alisema kuwa kikosi chake
kinaendelea vizuri na mazoezi ambapo kinamchanganyiko wa vijana na wakongwe
ambao wengine walikuwa kwenye timu zao za Taifa.
Maximo aliongeza kuwa beki aliyesajiliwa na timu hiyo,
Edward Charles ni mchezaji mzuri anayeamini ataisaidia Yanga kwa muda mrefu
kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Maximo anatarajia kutaja majina ya wachezaji ataokwenda
nao kwenye kambi kisiwani Pemba na watakaa huko kwa takribani siku kumi na
baadae kurudi Dar tayari kwa kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.