MAMLAKA ya usafiri na udhibiti wa nchi kavu na majini (Sumatra)
mkoa wa Mbeya imesema kuwa haitavumilia tabia ya baadhi ya watumiaji wa vyombo
vya usafiri kujaza mafuta wakati vikiwa vimebeba abiria.
Aidha mamlaka hiyo imesisitiza kuwa ikiwa watumiaji hao
watabainika kutenda kosa hilo watatozwa faini ya shilingi laki mbili na nusu.
Akizungumza na Highlands fm, Afisa mfawidhi wa Sumatra, Denis Daud
amesema vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa abiria na
kwamba mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa watumiaji hao.
Katika hatua nyingine Daud, amewataka watumiaji hao kujaza mafuta
ya kutosha kwenye magari yao ili kuondoa usumbufu kwa abiria pindi magari hayo
yanapokata mafuta barabarani.