Mrithi wa Sir Alex Ferguson Meneja wa klabu ya
Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa klabu hiyo imetuma ofa
nyingine kwa ajili ya kujaribu kumsajili Cesc Fabregas na kuonya kuwa
bado hajakata tamaa na kiungo huyo wa Barcelona. Akihojiwa na waandishi wa habari katika Uwanja wa Nissan jijini Yokohama,
Japan, Moyes amesema ofisa mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward bado anafanya
mawasiliano na Barcelona kuhusiana na Fabregas baada ya kutuma ofa ya
pili inayokadiriwa kufikia paundi milioni 30 ambayo itakuwa rekodi mpya
ya klabu kwenye usajili.
Moyes amedai kuwa ingawa wana wachezaji kadhaa ambao wako katika mipango yao kama usajili wa Fabregas ukishindikana lakini kwasasa bado hawajakata tamaa ya kupata saini ya nyota huyo. United kwasasa wako katika ziara yao ya tatu jijini Tokyo ambapo tayari nyota wake Shinji Kagawa, Ashley Young na Chris Smalling wameshaungana na wenzake baada ya kupona