Mshambuliaji nyota wa
klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya argetina Lionel Messi amempigia upatu kocha Gerardo Martino
kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo. Baada ya nafasi
ilikuwa wazi kutokana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Tito Vilanova
kulazimika kuachia ngazi kutokana na maradhi ya saratani yanayomsumbua.
Martino ambaye
aliiongoza timu ya Old Boys kushinda taji la Ligi Kuu chini Argentina
msimu uliopita ni mmoja wa makocha wanaoewa nafasi ya kuchukua nafasi ya
Vilanova na Messi ana imani kuwa kocha huyo anastahili nafasi hiyo. Messi
alidai kuwa Martino ni mmoja wa makocha wenye kiwango cha juu na kila
mtu anamheshimu hivyo haoni tatizo kama akikabidhiwa mikoba ya kuinoa
Barcelona.