URA ya Uganda kupitia uongozi wake umeamua kujajuu na kusema unashangazwa na kuiona inamtaka beki
Joseph Owino.
Meneja
wa URA, Sam Okabo amesema Simba walimuona mchezaji huyo hana thamani wakati
akiwa mgonjwa.
Simba
ilimuacha Owino ikiwa ni siku chache baada ya kubadilishana na Uhuru Selemani
ambaye alikwenda Azam FC.
Lakini
ikaonekana alikuwa hajapona vizuri hivyo viongozi wa Simba wakaamua kuachana
naye na kuanza kuhaha kusaka mabeki wengine.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope alimfuata Owino baada ya
mechi ya kirafiki dhidi ya URA ambayo Msimbazi walilala.