Nahodha wa club ya
Fc Barcelona, Carles Puyol amesema kuwa uamuzi wa Tito Vilanova kuachia ngazi
kuinoa klabu hiyo kuwa ni pigo kubwa. Vilanova
mwenye umri wa miaka 44 alitangaza kuachia ngazi wiki iliyopita ili
zweze kuendelea na matibabu yake ya saratani baada ya kuiongoza
Barcelona kunyakuwa taji la La Liga katika msimu wa 2012-2013.
Puyol
amekiri kuwa habari ya kujizulu kwa Vilanova imekuja kwa mshituko
lakini ameahidi kuonyesha kiwango cha hali ya juu msimu ujao ikiwa kama
sehemu ya kumshukuru kocha huyo. Beki
huyo ambaye msimu uliopita alikuwa akisumbuliwa na majeruhi amedai kuwa
wakati Vilanova akiwaaga aliwaomba kujituma kwa bidii katika msimu mpya
uliopo mbele yao na watafanya hivyo kwa heshima yake.