MOURINHO AMPASHA DAVID MOYES KUSAHAU KUMNASA C.RONALDO
The spesho one Kocha wa klabu ya
Chelsea, Jose Mourinho amemhabarisha meneja wa Manchester United, David
Moyes kusahau ndoto zake za kujaribu kumrejesha Cristiano Ronaldo Old
Traford. Kuna
tetesi kuwa United wako katika harakati za kujaribu kumrejesha nyota
huyo wa kimataifa wa Ureno pamoja na meneja mpya wa Real Madrid Carlo
Ancelotti kusisitiza kuwa hawatamuuza. Lakini
Mourinho ambaye msimu uliopita alikuwa akiinoa klabu hiyo amedai kuwa
hadhani kama Madrid wanaweza kumruhusu Ronaldo kuondoka kwasababu ya
uwezo mkubwa wa kifedha walionao kwasasa. Mourinho
amesema Madrid ni klabu tajiri duniani na hawana sababu ya kumuuza
nyota huyo hivyo wanaweza kukataa ofa yoyote itakayotolewa kwa ajili ya
kumchukua.