BOSI wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas ametanabaisha kuwa ni jambo la muhimu kwa klabu hiyo kumbakisha mshambuliaji wake nyota Gareth Bale kama wanataka kufanya vizuri zaidi msimu ujao. Spurs wamekosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika siku ya mwisho baada ya kuzidiwa kwa alama moja na mahasimu wao wa jiji la London Arsenal ambao walimaliza msimu katika nafasi ya nne. Kukosa huko nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya kumeleta mjadala kuhusu mustabali wa winga huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Wales. sambamba na hayo Villas-Boas amesema kama wanahitaji kufanya vyema msimu ujao ni lazima wawabakize wachezaji nyota na hilo ndio aliloambia na viongozi wa juu wa klabu hiyo. Bale amekuwa akifukuziwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ambavyo vitashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ikiwemo Real Madrid.