Tuesday, July 16, 2013

SIMBA YAJA NA MKUTANO MKUU JALAI 20 MWAKA HUU VS TBL"

Club ya soka ya Simba, inatarajia kufanya wake Mkutano Mkuu Jumamosi Julai 20 na Mdhamini wao, TBL, Tanzania Breweries Limited ambapo mdhamini huyo ametoa Shilingi Milioni 20 ili kuendesha Mkutano huo.
Mkutanno Mkuu huo ni fursa safi kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, kuwasilisha Ripoti ya shughuli za Klabu hiyo.
TBL, ambayo ina Mikataba ya Miaka mitano mitano ya kuzidhamini Yanga na Simba kuanzia Miaka miwili iliyopita, inawajibika kuzipa Klabu hizo Shilingi Milioni 20 kila mmoja ili kuendesha Mikutano Mikuu ya Vilabu vyao.
Akiongea wakati akikabidhi Cheki ya Shilingi Milioni 20 kwa Simba, George Kavishe, Meneja wa Bia ya aina ya Kilimanjaro Premium Lager, alisema: "Kama Wadhamini wakuu, tunatoa Fedha hizi kama jukumu letu kwa Klabu ili iwajibike, ipate mafanikio nje na ndani ya Uwanja. Tunaamini Mkutano huu utaimarisha uhusiano kati ya Simba na Wanachama wake kwa kuwapa nafasi kupitia masuala ya Klabu yao waipendayo."
Nae Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, aliishukuru TBL kwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Mkataba na akaahidi Fedha hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Kwa baadhi ya Wadau wa Simba Mkutano Mkuu huu unasubiriwa kwa hamu kubwa hasa baada ya Klabu hiyo kugubikwa na mfarakano na Mwezi Machi Kikundi kimoja cha waliodaiwa kuwa Wanachama kujaribu kumpindua Rage kwa madai ya kushindwa kuongoza lakini jaribio hilo halikufua dafu.
Pia, inasemekana ipo Kambi ya Wanachama itakayoshika bango waelezwe kinagaubaga nini kimetokea kuhusu kuuzwa kwa Straika wao kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, kwa Klabu ya Tunisia Etoile Sportive Du Sahel Mwezi Januari kwa Dau linalodaiwa kuwa Dola Laki 3 na Klabu kutolipwa Fedha hizo hadi sasa.
Wengine watapenda wajue nini kiliwasibu Msimu uliopita na kumalizika Mwezi Mei huku Simba ikinyang’anywa Taji lao la Ubingwa na Mahasimu wao wakubwa, Yanga, na pia kujikuta wakibwagwa hadi Nafasi ya 3 nyuma ya Yanga na Azam na hivyo kutopata fursa ya kucheza Mashindano ya Klabu Barani Afrika Mwakani.