Shirikisho la kandanda barani Ulaya-UEFA, limesema kuwa klabu za Fenerbahce na Besiktas za
Uturuki zimeshindwa rufani zao za kupinga adhabu ya kushiriki michuano
inayoandaliwa na shirikisho hilo. Fernabahce
ambao ilikuwa washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu
walifungiwa kushiriki michuano yoyote ya Ulaya kwa misimu miwili huku
Besiktas ambao walifuzu kushiriki michuano ya Europa League wao
wamefungiwa msimu mmoja. Klabu
zote mbili zinatuhumiwa na kashfa ya upangaji matokeo katika baadhi ya
mechi za Ligi ya Kuu ya Soka nchini Uturuki mwaka 2011. Baada ya kugonga mwamba UEFA, klabu hizo bado zina haki ya kukata rufani katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS.