Club ya Yanga ya jangwani kupitia uongozi wake
waumewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi
ya kimataifa ya kirafiki itakayochezwa Julai 18 mwaka huu.
Mechi hiyo kimataifa ya Kirafiki dhidi ya timu ya
3 Pillars ya Nigeria inataraji kutimua vumbi Julai 18 mwaka huu katika uwanja wa
Taifa.
Mechi
hiyo ni sehemu ya maandalizi ya klabu zote mbili kabla ya ligi kuu
kuanza mwezi ujao ambapo Yanga pia inajinoa kwa ajili ya michuano ya
ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mratibu
wa mechi Salum Mkemi amesema kikosi cha wachezaji 17 na viongozi na
makocha wao wapo jijini Dar es Salaam wakijifua kwa ajili mtanange huo
utakaochezwa katika uwanja wa Taifa.
Mkemi
amesema pia timu ya 3 Pillars ambayo imepanda daraja la ligi kuu nchini
Nigeria inataraji kujipima na Coastal Union ya Tanga huku wakifanya
mazungumzo na Mbeya City kwa ajili ya mechi nyingine za Kirafiki.
Katibu
mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amesema wachezaji wako kambini
kujiwinda na michuano ya ligi kuu na kuongeza kuwa wana morali kuelekea
mchezo huo.
Mratibu
wa mechi ametangaza Viingilio vya mechi hiyo vitakuwa kati ya shilingi
elfu tatu na elfu 15 ili kuwawezesha mashabiki wengi zaidi kuhudhuria
kipute hicho.
Timu ya 3 Pillars inataraji kurejea nchini Nigeria Julai 30 mwaka huu.