Shirikisho la kandanda Barani Afrika-CAF limesogeza mbele mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika
ambao unawakutanisha watani wa jadi nchini Misri timu za Zamalek na Al Ahly
mpaka Jumatatu ijayo.
Vigogo
hao wa soka nchini humo walitarajiwa kucheza Jumapili katika mji wa El
Gouna ambao uko kilometa 500 kutoka mji mkuu wa Cairo kutokana na sababu
za kiusalama. Katika
taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Zamalek, wamethibitisha kuwa FIFA
imekubali mchezo huo kuchezwa El Gouna pamoja na kwamba uwanja huo
haukuwepo katika ratiba za michuano hiyo na kuamua kuchelewesha mchezo
huo kwa siku moja kwasababu za kibiashara. Wizara
ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ilikataa mapema kuhakikisha usalama wa
mechi hiyo kuchezwa jijini Cairo au Alexandria kabla ya Zamalek kuchagua
El Gouna.
