LIGI KUU NCHINI MISRI YAWEKWA KAPUNI KWA SABABU ZA KIUSALAMA"
Ligi Kuu ya kandanda nchini
Misri imesimamishwa kwasababu za kiusalama kufuatia jeshi la nchi hiyo
kumuondoa rais Mohamed Mursi madarakani mapma mwezi huu. Shirikisho
la Soka la nchi hiyo lilitangaza rasmi kusitisha msimu wa ligi wa
2012-2013 huku kukiwa kumebaki mzunguko mmoja msimu kumalizika na timu
nne kucheza hatua ya mtoano kwa ajili ya kumpata bingwa. Kwa
zaidi ya wiki mbili toka jeshi limuondoe Mursi baada ya maandamano
makubwa ya kumpinga, kumekuwa na vurugu huku watu zaidi ya saba
wakiripotiwa kufa katika mapigano baina waislamu waliokuwa upande wa
Mursi na wengine waliokuwa wakimpinga rais huyo. Hii
ni mara ya pili katia kipindi cha miaka miwili ligi kusimamishwa
katikati ya msimu baada ya mapema mwaka jana ligi hiyo kusitishwa tena
kutokana na vurugu zilizotokea Port Said na kusababisha vifo vya
mashabiki wapatao 74.