MWAMBUSI ASEMA PHIRI, MAXIMO, ASEMA NGOMA DAKIKA 90.
KOCHA mkuu wa Mbeya City
fc na kocha bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita, Juma
Mwambusi, amewakaribisha makocha Patrick Phiri wa Simba na Marcio Maximo
wa Yanga.
Akizungumza na mtandao huu,
Mwambusi amesema kocha Phiri ana historia ya kufundisha soka la Tanzania
kwa ngazi ya klabu wakati Maximo amefundisha timu ya Taifa, lakini wote
wataleta changamoto nzuri kwake.