Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT)
limesogeza tarehe ya kufanyika kwa mashindano ya ngumi ya Taifa na sasa
yatafanyika kuanzia tarehe 03-08/11/2014.Dar es salaam.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika tarehe 08-14/10/2014 Dar es salaam.
Sababu za kusogeza mashindano hayo
ni kuyapisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yaliyoandaliwa na chama
cha ngumi wilaya ya Temeke yanayotarajia kuanza kufanyika mwishoni mwa
mwezi huu, lakini pia ni kutoa nafasi zaidi kwa mikoa ili kujiandaa
vizuri na kufanya mashindano ya kuwapata wawakilishi wa mikoa yao katika
mashindano ya taifa.
BFT tunawataki maandalizi mema na tunatoa wito kwa maafisa michezo
wa mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha wanaleta wachezaji kutoka
katika mikoa yao ili kuleta upinzani utakaopelekea kupata timu ya taifa
iliyo bora kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Aidha BFT inawapongeza kampuni ya
simu za mkononi ya Z antel kwa udhamini wa mashindano hayo kwa
kutoa kiasi cha Tsh. 10,000,000/=ambazo zitasaidia baadhi ya mahitaji ya
msingi ya kufanikisha mashindano hayo.