HUKUMU YA SUAREZ CAS KUJULIKANA KESHO.
MAHAKAMA ya Kimataifa ya
Usuluhishi ya Michezo-CAS imedai kuwa hatma ya rufani ya mshambuliaji
nyta wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez kupinga adhabu aliyopewa kwa
kumng’ata Giorgio Chiellini itajulikana kesho. Suarez alifungiwa mechi
tisa za kimataifa na kutojishughulisha na mambo yoyote yahusuyo soka kwa
miezi minne baada ya kufanya tukio hilo katika mchezo wao wa hatua ya
makundi. Italia
kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Baada ya kushindwa rufani yake kwa
Shirikisho la Soka Duniani-FIF, mshambuliaji huyo wa Barcelona alipeleka
kesi hiyo CAS ambayo ilisikiliza shauri hilo Ijumaa iliyopita. Katika
taarifa yake CAS ilithibitisha kuwa itatoa uamuzi wake kuhusiana na
rufani hiyo kesho.