Wednesday, August 13, 2014

PHIRI ATUA JIJINI DAR KUJIUNGA WA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Mzambia Patric phiri atua jijini dar es salaam lengo likiwa ni kufanya mazungumzo ya kina na uongozi wa club hiyo ili kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC ambayo hivi karibuni ulimtupia virago alikuwa kocha mkuu Logarusic.

Akitua katika viwanja wa JK nyerere hii leo mashabiki wachache walitokeza kumpokea kocha huyo hivyo asilimia kubwa ya phiri ndie atakuwa kocha mkuu wa simba kwa msimu ujao wa ligi kuu vodacom tanzania bara unao tarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo september 20 mwaka huu.
Katika akifundisha simba Phiri aliwahi kuwa Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam wiki hii kwa ajili Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi zake.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Kiboko ya Yanga anarudi; Patrick Phiri anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa kusaini Simba SCMazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Phiri na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.
Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji.

Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana. 
Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.