
Amri
hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa
ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007. Hadi sasa
tumeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.
Jitihada zinafanyika ili kumaliza deni hilo. Pia tunachunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.
CAF YAZUIA MECHI ZAKE KUPISHA EBOLA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limezuia mechi zake kuchezwa Guinea,
Liberia na Sierra Leone kutokana na kuripotiwa kuwepo kwa wagonjwa wengi
wa Ebola katika nchi hizo.
Ikiwa
ni njia mojawapo ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo kupitia
mkusanyiko wa watu, CAF imevitaka vyama vya mpira wa miguu vya nchi hizo
kuchagua viwanja vingine huru kwa ajili ya timu zao zinazoshiriki
michuano yake kwa kipindi hiki hadi katikati ya mwezi ujao.
CAF
itafanya tathmini nyingine kuhusiana na ugonjwa huo kuanzia katikati ya
Septemba ili kuona kama nchi hizo zinaweza kupokea timu ngeni kwa ajili
ya mechi mbalimbali za michuano yake, na baadaye kufanya uamuzi wa
kuruhusu au kuendelea kusimamisha.
Pia
kutokana na mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), CAF imesema
kwa nchi zenye virusi vya Ebola ni muhimu kwa vyama vyake vya mpira wa
miguu kuufanyia vipimo vya afya msafara wa timu zao ili kuhakikisha
wenye virusi vya ugonjwa huo hawasafiri.