Monday, August 18, 2014

FIFA KUBORESHA MAKAO MAKUU YA TFF

ofisi-za-TFFSHIRIKISHO la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa ofisi.
Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.