KIUNGO nyota wa klabu ya
Barcelona Cesc Fabregas amekanusha na kutanabaisha kuwa tuhuma za kwamba anataka kurejea jijini London
nchini Uingereza baada ya kukosa namba ya kudumu katika klabu hiyo. Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Barcelona mwaka 2011 lakini
Manchester United na klabu yake ya zamani ya Arsenal wanaaminika kutaka
kumchukua mchezaji huyo kutoka Camp Nou. Fabregas
amesema siku zote amekuwa na furaha Barcelona na yoyote anayesema
kwamba anataka kuondoka hamjui na hajawahi kuzungumza nae.
Kiungo huyo ametokea katika shule ya vipaji ya Barcelona akiwa na miaka 10 mpaka 16 alisajiliwa na Arsenal, na ameichezea klabu hiyo mechi 303 kwa kipindi cha miaka nane na kufanikiwa kufunga mabao 57.