
Mchezaji huyo kutoka Argentina na
babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa kujaza fomu
zisizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na 2009.Hata hivyo
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
Messi hulipwa Euro milioni
kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi
duniani.Lakini mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za
mahakama nyumbani kwa mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini
Barcelona.
Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha
malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.Messi na
babake wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ng’ambo, mjini Belize na
Uruguay kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa
kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Hispania, ambako anaishi na kucheza soka
ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa paundi milioni tatu na nusu.