LAPORTA AMKINGIA KIFUA MKALI WA DUNIA -MESSI
RAIS wa zamani wa
mabingwa wa Hispania, Barcelona Joan Laporta amemkingia kifua nyota wa
klabu hiyo Lionel Messi dhidi ya tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili. Laporta
ambaye ameiongoza Barcelona kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 aliiambia
radio moja nchini humo kuwa ana uhakika kuwa si Messi wa baba yake
wamefanya kitedo hicho. Messi
na baba yake Jorge wameshitakiwa na jana na mwendesha mashtaka Raquel
Amado wa mji wa Gava uliopo karibu na Barcelona ambapo anaishi nyota
huyo, kwa kosa kukwepa kodi inayofikia kiasi cha euro milioni 4.1 kati
ya mwaka 2007 na 2009. Laporta
amesema hakumbuki katika kipindi chake chote cha uongozi kama nyota
huyo alikuwa akijishughulisha na makampuni yasiyo halali, na anachojua
yeye Messi aliyofautiana na mmoja wa washauri wake hivyo anadhani tuhuma
hizo zimetoka huko.