CHELSEA YAMNASA MBADALA WA COLE KUTOKA ATLETICO.
KLABU ya Atletico Madrid
imetangaza kuwa imefikia makubaliano na Chelsea kuhusu uhamisho wa
Filipe Luis. Chelsea kwa kipindi kirefu amekuwa wakihusishwa na kutaka
kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 huku mwezi Juni wakiipa
taarifa Atletico kuwa wako tayari kutoa paundi milioni 20 zilizowekwa
katika mkataba wake. Atletico wamethibitisha rasmi kuwa wameshakubaliano
juu ya uhamisho huo na kilichobakia ni mchezaji huyo kufanyiwa vipimo
vya afya na Chelsea. Luis anatarajiwa kuziba nafasi ya Ashley Cole
aliyeruhusiwa kuondoka kwenda Roma kama mchezaji huru kufuatia
kumalizika kwa mkataba wake. Beki huyo wa kushoto atajiunga na mchezaji
mwenzake Diego Costa ambaye naye alikamilisha usajili wake kutoka
Atletico uliogharimu kiasi cha paundi milioni 35 mapema wiki hii. Luis
anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki cha
majira ya kiangazi baada ya kusajiliwa kwa Costa, Cesc Fabregas na
kiungo chipukizi Mario Pasalic.