MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu kutoka nchini Uingereza, Luol Deng amejiunga na timu ya Miami Heat kama mchezaji huru. Deng ambaye amezichezea timu za Cleveland Cavaliers na Chicago Bulls msimu
uliopita anatarajiwa kuchukua nafasi ya LeBron James
ambaye amehamia Cavaliers wiki iliyopita. Rais wa Heat, Pat Riley
amesema Deng ni mmoja ya mchezaji muhimu waliomsajili katika historia ya
timu hiyo. Deng ambaye ni mzaliwa wa Sudan aliiwakilisha Bulls kutoka
mwaka 2004 mpaka 2014 na mara mbili amefanikiwa kuchaguliwa katika
kikosi cha wachezaji nyota wa mchezo huo nchini Marekani, aliuzwa
Cavaliers Januari mwaka huu. Heat wamefanikiwa kutinga fainali nne
zilizopita za Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani-NBA ambapo
walishinda mwaka 2012 na 2013 lakini walichapwa na San Antonio Spurs msimu uliopita.