Wakati Jose Mourinho akijisifia kwamba timu bora imeshinda, kocha wa
Liverpool Brendan Rodgers akiongea na waandishi wa habari ameipaka timu
ya Chelsea kwa aina ya uchezaji wao.

Kocha wa Liverpool amesema Chelsea walipaki mabasi mawili golini kwao na ilikuwa ni vigumu kwa wao kupita kujaribu kupata goli.
Licha ya ushindi huo mashabiki wengi wa soka kwenye mtandao wa
goal.com wakati post hii inawekwa wameipa nafasi kubwa Manchester
city(44.4%) kuchukua taji hilo. Kura hizo zimeipa Liverpool(41%) nafasi
ya pili na kumaliza na Chelsea(14.6%).