Msimu uliopita, kipindi kama hiki, Luis
Suarez alikuwa akianza kutumikia Adhabu ya Kifungo cha Mechi 10 baada
kumuuma Meno Mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic, lakini safari hii
ni kidedea.
Suarez alikabidhiwa Tuzo yake Jana Usiku
kwenye Hoteli ya Kifahari, Grosvenor House, Jijini London mara baada ya
kuruka kutoka Jijini Liverpool baada ya Mechi yao Uwanjani kwao Anfield
walikofungwa Bao 2-0 na Chelsea.
Msimu huu, Suarez amefunga Bao 30 katika Mechi 31 za Ligi licha ya k
uzikosa Mechi za mwanzo wa Msimu akiwa bado Kifungoni.
Mchezaji wa Chelsea, Eden Hazard, ambae
hakucheza hiy
o Jana huko Anfield, alitwaa Tuzo ya England ya Mchezaji
Bora Kijana wa Mwaka ya PFA.

Chelsea pia walikuwa na Wachezaji watatu ambao ni Petr Cech, Gary Cahill na Hazard.
Manchester City inawakilishwa na Vincent Kompany na Yaya Toure huku Southampton ikiwa na wawili, Luke Shaw na Adam Lallana.
Mabingwa Watetezi, Manchester United nar Arsenal, haina hata Mchezaji mmoja.
PFA-LIGI KUU ENGLAND-TIMU YA MWAKA:
Petr Cech (Chelsea); Luke Shaw (Southampton), Vincent Kompany
(Manchester City), Gary Cahill (Chelsea), Seamus Coleman (Everton); Eden
Hazard (Chelsea), Yaya Toure (Manchester City), Steven Gerrard
(Liverpool), Adam Lallana (Southampton); Luis Suarez (Liverpool), Daniel
Sturridge (Liverpool)
WANASOKA BORA WA MWAKA ENGLAND
Mchezaji Bora wa Mwaka: Luis Suarez (Liverpool).
Mchezaji Bora Chipukizi wa mwaka: Eden Hazard (Chelsea).
Mchezaji Bora wa kike wa Mwaka: Lucy Bronze (Liverpool Ladies).
Mchezaji Bora chipukizi wanawake: Martha Harris (Liverpool Ladies).
Mchezaji Bora Chipukizi wa mwaka: Eden Hazard (Chelsea).
Mchezaji Bora wa kike wa Mwaka: Lucy Bronze (Liverpool Ladies).
Mchezaji Bora chipukizi wanawake: Martha Harris (Liverpool Ladies).