Tuesday, October 14, 2014

SIMBA KESHO KUONYESHANA KAZI NA JOMO COSMOS THN KURUDI DAR

Timu ya simba wekundu wa MSimba kesho inataraji kushuka dimba kupapatuana katika mechi yake ya mwisho ya kirafiki kesho dhidi ya Jomo Cosmos.

Mechi hiyo itapigwa jijini Johannesburg na baada ya hapo Simba itaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi dhidi ya watani wake Yanga, Oktoba 18.
Wekundu hao tayari Simba wamecheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Orlando Pirates ambayo ilitoka sare ya ya bila kufungana kabla ya kupata kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa Wits.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji amewataka mashabiki wa Msimbazi kutotegemea mambo makubwa sana katika mechi yao ya Oktoba 18 dhidi ya Yanga.

Dewji ambaye yuko Johannesburg, Afrika Kusini ambako kikosi cha Simba kimeweka kambi, amesema bado kuna mambo mengi yanapaswa kubadilishwa.