Saturday, November 1, 2014

JUMUIYA YA WAZAZI YA(CCM) MKOA WA DAR YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.
Moto huo ameutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Alisema kwa mfano katika shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga kuwa ina ardhi ya kutoka lakini haifanyiwi uzarishaji mali wowote.
Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo kwani litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli za maendeleo.
Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono rasimu ya Katiba mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalumu na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania. 
Ametoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.
Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia hiyo kiutendaji badala ya kuegemea katika eneo moja la siasa.