SERIKALI ya Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa miaka 50 wamakubaliano wa mradi wa pili wa kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye kituo cha Rusumo.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo, alisema mkataba huo umezihusisha nchi mbili ambapo alibainisha kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza katika sehemu ya mwisho ya kutekeleza mradi wa kwanza ulioanza mwaka jana yapo baadhi ya maeneo nchini yatapata umeme.
Alisema kupitia mradi huo nchi itaweza kuimarisha grid ya Taifa na kupunguza tatizo la umeme kwenye maeneo mengi nchini.
Kuhusu ujenzi wa mfumo wa usafirishaji umeme alisema kila nchi itajitegemea katika kusafirisha umeme na kubainisha kuwa Tanzania itajenga mfumo huo kuanzia miaka michache ijayo.
Hata hivyo Prof. Muhongo hakubainisha kiasi halisi kitakacho tumika kuendeshea mradi huo wa wamu ya pili