ASKARI polisi wa kitengo cha usalama
barabarani Wilayani Chunya Mkoani Mbeya, PC Zeferin Didas Focas mwenye
umri wa miaka (34) amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya raia Abisai
Wadi mwenye miaka 22.
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya,
Ahmed Msangi, amethibitisha kufukwa kazi kwa askari huyo baada ya husika na mauji
ya raia huyo yaliyotokea katika Kata ya
Igalula barabara ya Itindi Mkwajuni Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema, askari huyo akiwa na
mwezie aliisimamisha pikipiki iliyokuwa imempakia abiria nyuma ambapo dereva
huyo alikaidi, ndipo askari huyo alichukua jiwe na kuitupia pikipiki hiyo
iliyokuwa katika mwendo kasi na kumpata abiria huyo.
Amesema, jiwe hilo linasemekana
lilimkuta abiria aliyepakizwa kwenye poikipiki hiyo lakini haikuwekwa wazi
kwamba jiwe hilo lilimpata katika sehemu ipi ya mwili wa marehemu huyo.
Amesema, askari huyo ambaye kwa sasa
anatambulika kwa namba ya X6710 anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili
kujibu tuhuma za mauji zinazomkabili mbele yake.