Wednesday, November 26, 2014

SERIKALI YATOA SH. BILIONI 5 KIANZIO UJENZI WA JENGO LA MAABARA YA UPASUAJI.

JUMLA  ya shilingi  bilioni tano  zimetolewa  na serikali  kama kianzio cha ujenzi wa jengo la upasuaji  ujenzi wa maabara pamoja na kununua dawa katika hospitali teule ya rufaa  ya Tumbi mkoani Pwani.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanri mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu ambapo amekiri kuwa miundombinu ya hospitali hiyo haiendani na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa hospitali hiyo, ambapo inakadiriwa shilingi bilioni 30 zilitumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi huo kwa mwaka 2010.