TIMU ya taifa ya Libya
wametawadhwa mabingwa wapya wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wa ndani, CHAN baada ya kuifunga Ghana kwa changamoto ya
mikwaju ya penati katika mchezo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa
Cape Town nchini Afrika Kusini. Libya walinyakuwa taji lao hilo la
kwanza la kihistoria kwa kuigaragaza Ghana kwa penati 4-3 baada ya
mchezo huo kumalizika bila ya kufungana mpaka katika muda wa nyongeza.
Hiyo inakuwa mechi ya tatu kwa Libya kushinda kwa changamoto ya mikwaju
ya penati baada ya kuziengua Gabon na Zimbabwe katika hatua ya robo
fainali na nusu fainali. Kwa wa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu
Nigeria walifanikiwa kuibuka kidedea baada ya kuifunga Zimbabwe kwa bao
1-0.