TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.

TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.
Pia Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi.

TFF inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.
TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo.
Wakati huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.
JAMAL MALINZI
RAIS
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)