Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais
wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.

Ameongeza kuwa Grondora alikuwa
mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia
mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo
utaendelea kukumbukwa wakati wote.
Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole
kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.