Sunday, November 23, 2014

RONALDO NAE YU MBIONI KUVUNJA REKODI LA LIGA"MESSI SAFI

WAKATI Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi Jana akivunja Rekodi na kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya La Liga, Cristiano Ronaldo yuko mbioni kuivunja Rekodi ya kufunga Bao nyingi katika Msimu mmoja wa Ligi hiyo ambayo inashikiliwa na Messi.
Messi aliweka Rekodi ya Bao nyingi katika Msimu mmoja kwenye Msimu wa 2011/12 alipofunga Bao 50.
Lakini Jana Ronaldo alifunga Bao 2 wakati Timu yake Real Madrid inaichapa Eibar Bao 4-0 na sasa amefikisha Bao 20 katika Mechi 11 za La Liga Msimu huu kwa jinsi mwendo wake wa kufunga Mabao ulivyo Msimu huu Wachambuzi wanahisi Ronaldo, ambae ni Mchezaji Bora Duniani, anao uwezo wa kufunga zaidi ya Mabao 60 kwa Msimu huu.
Tayari Ronaldo, mwenye Miaka 29, ameweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza katika Historia ya La Liga kufikisha Bao 20 katika Raundi 12 za mwanzo za Ligi za Msimu huu.
Tangu ajiunge na Real kutoka Manchester United Mwaka 2009, Ronaldo amefunga Mabao 197 kwa Mechi 176 za La Liga na Messi Mabao 253 katika Mechi 289 kuanzia 2004 ambayo ndio hiyo Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya La Liga.
Lakini pia vita hii ya Rekodi za Magoli kati ya Ronaldo na Messi zitaendelea tena kati Wiki wakati Real na Barcelona zitakapojikita kwenye Mechi za 5 za Makundi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Kwenye UCL, Messi amefunga Bao 71 sawa na Mchezaji wa zamani wa Real, Raul, na wao ndio wanaongoza Kihistoria katika Ufungaji Bora kwa Ulaya lakini Ronaldo akiwa na Bao 70 yuko nyuma kwa Bao 1.
Jumanne Barcelona wako Ugenini huko Cyprus kucheza na Apoel Nicosia na Jumatano Real nao wako Ugenini kucheza huko Uswisi na FC Basel.