Uongozi
wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye
mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale
kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young
Africans Bw Yusuf Manji alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na
kua chanzo cha migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali
likiwa halina hadhi ya kuwa Tawi Kamili.

Ibara
ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za uanachama kwa
muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum inayokubalika na
Kamati ya Utendaji"
Baadhi ya Wanachama walijifuta
uanchama wao kutokana na kushindwa kulipia ada zao za uanachana kwa
kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama inavyojieleza kwenye Katiba kwamba
mwanachama asipolipia ada yake zaidi ya miezi sita moja kwa moja
anajifuta uanachama wake.
Hivyo Uongozi wa klabu
ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote watambue kuwa
Tawi la Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku
wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia
ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho
wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama
mapema kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa
marekebisho ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -
Oysterbay Juni Mosi 2014.
Beno Njovu
Katibu Mkuu - Yanga SC
Mei 23, 2014