TAIFA STARS, MALAWI KUONESHANA SHUGHULI DAR, KIINGILIO BUKU 5 TU!
Taifa Stars na Malawi (Flames)
zinapambana kesho (Mei 27 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki ya
kimataifa itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11
kamili jioni.
Malawi tayari ipo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya mechi hiyo wakati Taifa Stars iliyopiga kambi yake
Tukuyu mkoani Mbeya inawasili jijini Dar es Salaam kesho (Mei 27 mwaka
huu) saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Tanzania.