Thursday, April 18, 2013

WANANDINGA WA KIAFRIKA KATIKA SOKO LA ULAYA

Wachezaji wa Kiafrika wazidi kupata soko Barani Ulaya hivyo Watanzania wasichezee fursa ya soka la kimataifa.
v  Zaidi ya Mawakala 15 wawasiliana na Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji 
 Zaidi ya mawakala 15 tayari wamewasiliana na Kampuni ya Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji mbalimbali kwaajili ya kuwapeleka kwenye klabu za barani Ulaya, Asia na Afrika ili kucheza soka la kulipwa.

Mwitikio huo umeongezeka kutokana na vijana wa kiafrika kuwa na soko kubwa katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu kwa nchi mbalimbali kama Sweden, Uholanzi, Denmark, Ureno na nchi nyinginezo.

Arne Anderson kutoka AA Football Service ya Sweden amesema kuwa binafsi yuko tayari kuchukua wachezaji wawili kwaajili ya kuwatafutia clubs nchini humo kwani tayari mafanikio ya wachezaji watano wa kiafrika aliowapeleka yamempa maombi ya timu nyingi za Sweden.

“Niko tayari kuchukua wachezaji wawili endapo tutakubaliana kuhusu maslahi yangu pindi wachezaji hao wakianza kucheza hapa”, Arne amesema.

Kutokana na mafanikio hayo na maombi ya mawakala lukuki Kampuni ya Tanzania Mwandi inazidi kuwasisitizia wachezaji wa Kitanzania kujaza fomu zinazopatikana kupitia blog.tanzaniamwandi.co.tz ili kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Sweden, Norway, Denmark, Uholanzi, Ureno, Uswiss, Ufaransa na Ubelgiji, barani Asia (Kuwait, China, Qatar nk) na klabu nyingine barani Afrika.

Mpaka sasa jumla ya wachezaji wa kitanzania 15 wamekwishajaza fomu za haraka kwenye tovuti ya Tanzania Mwandi huku kampuni ikiwa imepokea pia maombi ya wachezaji 25 kutoka nje ya nchi.

“Maombi yanazidi kuja ingawa tunawahimiza Watanzania wasikimbie kiingilio cha shilingi 300, 000 wakumbuke kuwa wanafanya majaribio wakiwa nyumbani na watakapopata timu Kampuni ya Tanzania Mwandi haitachukua chochote kwenye mikataba yao, ni wao na mawakala ndio watakokubaliana juu ya watakachokipata kutoka kwa klabu husika”, alisema Teonas Aswile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, waandaaji wa African Youth Football Tournament.

Aswile amezialika klabu mbalimbali za ligi kuu ya soka Tanzania Bara na Visiwani kutazama wachezaji watakaofika katika michuano hiyo kwani wapo baadhi ya wachezaji kutoka nje ya nchi ambao watafika na wangependa kucheza soka la Tanzania.

“Kati ya wachezaji 25 wa nje ya nchi wengine wameomba tuwatafutie timu hapa nchini hivyo klabu zikija zinaweza kuwapata wachezaji hao wakiwa huru kwasababu watakuja kwa gharama zao kufanya majaribio nchini. Pia klabu hizo zitumie fursa hii kuuza wachezaji wake.”
Michuano ya African Youth Football Tournament inatarajia kufanyika Juni 10 hadi 14 mwaka huu katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kati ya miaka 18 hadi 21 kutoka Tanzania na bara zima la Afrika. Taarifa zaidi kuhusu michuano hiyo zinapatikana kupitia;  blog.tanzaniamwandi.co.tz  
Imetolewa na Idara ya Habari
Kampuni ya Tanzania Mwandi,
TANCOT House, Ground Floor,
S. L. P 79944,
Dar es Salaam.
MECHI YA MGAMBO, YANGA YAINGIZA MIL 24/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mgambo Shooting na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 17 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga imeingiza sh. 24,865,000 kutokana na watazamaji 4,386.

Viingilio katika mechi hiyo namba 162 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 vilikuwa sh. 10,000 kwa jukwaa kuu na sh. 5,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 5,547,337.50 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,792,966.10.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 2,820,680.08, msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 90,000, waamuzi sh. 270,000, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 1,587,500.

Mgawo mwingine ni gharama za mechi sh. 1,692,408.05, Kamati ya Ligi sh. 1,692,408.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 846,204.05 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) sh. 658,158.69.

MAKOCHA AZAM, FAR RABAT KUTETA
Makocha wa timu za Azam, Stewart John Hall na AS FAR Rabat ya Morocco, Abderazzak Khairi watakutana na waandishi wa habari kesho (Aprili 19 mwaka huu) kuzungumzia mechi yao itakayofanyika Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao pia utawahusisha manahodha wa timu hizo mbili utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Barabara ya Uhuru na Shaurimoyo.

Timu hizo zitakutana katika mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho itakayoanza saa 10 kamili jioni. Mechi ya marudiano itachezwa nchini Morocco wiki mbili baadaye.

JKT RUVU, YANGA KUUMANA JUMAPILI
Yanga ambayo inafukuzia kwa karibu taji la Ligi Kuu ya Vodacom itapambana na JKT Ruvu katika mechi pekee ya ligi hiyo wikiendi hii itakayofanyika Jumapili (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa mwezi huu ni kati ya African Lyon na JKT Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nayo Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja wa Taifa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Simba na Polisi Morogoro itakayofanyika Aprili 28.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAMBO YA NDONDI - CHALINZE
WANANDONDI Mwaite Juma,Cosmas Kibuga na Shabani Kaoneka ni baadhi ya mabondia wa Dar es salaam watakaokwenda Chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa Chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi ya Bigright Promotion, imeandaa pambano hilo ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimichezo ikiwemo wilaya ya Chalinze.

Tumeamua kuifanyia Chalinze kwa sababu tunataka iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa Dar na wakali wa Chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu.
ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda kushangilia na kurudi.

wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wa ngumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo
LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA

MSIMAMO:

NA
TIMU
p
W
D
L
GD
PTS
1 
YANGA 
23
16
5
2
28
53
2
Azam FC
23
14
5
4
22
47
3
Kagera Sugar
23
10
7
5
7
40
4
Simba
22
9
9
4
11
36
5
Mtibwa Sugar
24
8
9
6
2
36
6
Coastal Union
23
8
8
6
3
33
7
Ruvu Shooting
22
8
6
8
0
30
8
JKT Oljoro
24
7
7
9
-4
28
9
Prisons FC
24
6
8
10
-7
26
10
Mgambo Shooting
23
7
4
12
-7
25
11
Jkt RUVU
23
6
4
11
-15
23
12
Toto african
25
4
10
10
-12
22
13
Police M
23
3
10
10
-10
19
14
African Lyon
23
5
4
14
-19
19

MATOKEO  JANA

Aprili 17, 2013

Mgambo JKT 1-1 Yanga SC

Kagera Sugar 1-0 Toto Africans

Mtibwa Sugar 1-0 JKT Oljoro

MECHI ZILIZOBAKI VPL
Aprili 21, 2013
JKT Ruvu Vs Yanga SC
Aprili 25, 2013
Ruvu Shooting Vs Simba SC
African Lyon Vs JKT Ruvu
Aprili 27, 2013
Coastal Union Vs Azam FC
Aprili 28, 2013
Simba SC Vs Polisi Moro
Mei 1, 2013
Mtibwa Sugar Vs African Lyon
Yanga SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs TZ Prisons
Polisi Moro Vs Kagera Sugar
Ruvu Shooting Vs JKT Oljoro
Mei 8, 2013
Simba SC Vs Mgambo JKT
Mei 11, 2013
Azam FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting
Mei 18, 2013
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
HATARINI KUSHUKA DARAJA:
1.Polisi moro
2.African lyon
3.Toto african
4.Jkt ruvu
KUZIPISHA TIMU ZILIZO PANDA MSIMU UJAO
1.Mbeya city
2.Ashanti united
3.Rhino rangers
WAARABU WAJA NA VITUKO KEDEKEDE


TIMU ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayoikabili Azam kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho imetua jana (Aprili 17 mwaka huu) saa 7.30 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.

Wapinzani hao wa Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, AS FAR Rabat ya Morocco baada ya kuwasili jana Dar es Salaam wameanza na vituko kedekede.
kwanza wamijawa na  wasiwasi tangu wanatua katika dimba la Uwanja wa Ndege na kutoa imani kwa  wapinzani wao, wakikataa mapokezi na mwishowe  kukataa hoteli waliyokodiwa na wenyeji wao, Sapphire Court.
Pamoja na kuambiwa hoteli hiyo imepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na timu zote zilizocheza na Azam katika mashindano hayo, zilifikia hapo, Al Nasir ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers II ya Liberia, lakini wakagoma.
Wenyeji wakawaambia kama hawataki hoteli hiyo watajilipia popote watakapokwenda na Waarabu hao nao wakaonyesha jeuri ya fedha kwa kujipangia New Africa Hotel. Kaazi kweli kweli.
ukitafakari kwa undani zaidi ni moja ya dalili mbaya kwa Waarabu hao kugomea hoteli na visa vyote walivyofanya, hata hivyo ni hatari kwa Azam  katika wakielekea  Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Azam watakwatuana na timu hiyo ya far rabat {Waarabu hao} Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Morocco na mshindi wa jumla ataingia kwenye droo ya kucheza na timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 
Azam FC ilifanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuichalaza magoli 2-1 Barack Young Contollers II ya Liberia.Ilianza kwa kushinda 2-1 mjini Monrovia kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.

Tuesday, April 16, 2013

KAMATI  MAALUM YAUNDWA KUHUSU TAIFA STAR "

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyobakia ya kufuzu michuano ya Kombe la dunia 2014. Hivi karibuni Stars ilifanikiwa kuitandika Morocco mabao 3-1 hivyo kufanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi C walilopo wakiwa na timu zingine za Ivory Coast na Gambia. Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa Stars wako katika nafasi ya pili wakiwa na point sita, nyuma ya vinara Ivory Coast wanaoongoza kwa alama saba na Morocco ni ya tatu wakiwa na alama mbili wakati Gambia wao wanashikilia mkia wakiwa na alama moja. Kutokana na matokeo hayo wizara kupitia waziri wake Fenela Mukangara wameipongeza timu hiyo kwa kuweka matumaini hai ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. na kwa kuzingatia hilo wizara imeamua kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kuongeza hamasa ya ushindi kwa Stars ili iweze kuweka historia kwa kushiriki michuano ya Brazil. Jukumu la msingi la Kamati iliyoundwa ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi.star kwa sasa katika viwango vya fifa ipo katika nafasi ya 116

Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-


Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
Bi. Teddy Mapunda - Montage
Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
Bw. George Kavishe - TBL
Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw. Joseph Kusaga - Clouds
Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge
Kamati hiyo iliyoteuliwa leo, inatakiwa kuanza kazi kazi mara moja. Hadidu za rejea zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa. Serikali inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TFF_LOGO12Aprili 16, 2013
RAMBIRAMBI MSIBA WA MEJA JENERALI MAKAME RASHID
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame Rashid kilichotokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi jijini Dar es Salaam.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo kuwa mlezi wa timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa Kikosi cha Ruvu JKT.
Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini (Trustee) wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) na wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa ndiyo kwanza imepanda kucheza Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani Mtwara. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina
VPL KUTIMUA VUMBI VIWANJA VITATU
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 17 mwaka huu) kwenye viwanja vitatu huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakifukuzia ubingwa huo jijini Tanga.
Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 52 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Athuman Lazi kutoka Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo ni Michael Mkongwa wa Iringa na Godfrey Kihwili wa Arusha wakati Kamishna wa mechi hiyo ni Godbless Kimaro kutoka Moshi.
Kagera Sugar na Toto Africans zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mechi namba 164 itakayokuwa chini ya mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro.
Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro, na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 4,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mtibwa Sugar yenye pointi 33 na Oljoro JKT yenye pointi 28.
Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Hamis Chang’walu (Dar es Salaam) na John Kanyenye (Mbeya). Kamishna wa mechi hiyo ni Ramadhan Mahano kutoka Iringa.
AS FAR KUWASILI KESHO KUIKABILI AZAM
Wapinzani wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)