Friday, April 19, 2013

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 12

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata.
Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
KILA LA KHERI AZAM FC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam FC katika mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kesho (Aprili 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Azam FC ina fursa nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelisheli kutokana na maandalizi iliyofanya, lakini vilevile tunatoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono.
Makocha wasaidizi wa timu zote mbili, Kalimangonga Ongala wa Azam na Lahcen Ouadani wa AS FAR Rabat wamezungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi hiyo, kuwa wamejiandaa kuibuka na ushindi.
Kocha Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.
Naye Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jijini Dar es Salaam Machi 24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1.
Baadhi ya wachezaji ambao Azam inatarajia kuwatumia kwenye mechi ya kesho ni pamoja na Aishi Manula, Mwadini Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum Abubakar ambao pia wamo kwenye kikosi cha sasa cha Taifa Stars kilicho chini ya kocha Kim Poulsen.
AS FAR Rabat ina wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji hao ni mabeki Younes Bellakhdar, Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal, na viungo Salaheddine Said, Salaheddine Aqqal na Youssef Kaddioui.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Thursday, April 18, 2013

LYBIA KUTENGA MADOLA KATIKA UJENZI WA VIWANJA
WAZIRI Mkuu Msaidizi wa Libya Awad Ibrahim Elbarasi amesema serikali ya nchi hiyo imepanga kuwekeza kiasi cha dola milioni 314 kwa ajili ya ujenzi wa viwanja mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2017 kwa mategemeo kwamba michuano hiyo itawaunganisha wananchi baada ya vita ya mwaka 2011. Elbarasi amesema kama ilivyokuwa kwa Nelson Mandela alivyofanya nchini Afrika Kusini ni mategemeo yao wataiunganisha Libya kwa kutumia michuano hiyo. Waziri huyo aliendelea kusema kuwa ujenzi kwa ajili ya viwanja hivyo vipatavyo 11 unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu na tayari fedha hizo zimekwishaombwa serikalini. Mwezi uliopita Libya ilidai kuwa itatumia rasilimali zake zote kuhakikisha wanalinda haki yao ya kuandaa michuano ya 2017 baada ya kushindwa kuandaa michuano ya Afrika ya mwaka huu na vita.

BARCELONA USO KWA USO NA NEYMA
KLABU ya arcelona imeonekana kukaribia kumnyakuwa nyota wa klabu ya Santos, Neymar baada ya klabu hiyo kupanga kuanza kufanya mazungumzo naye Julai mwaka huu. Neymar mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akisisitiza kuwa anataka kubakia katika klabu yake ya Santos mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 lakini amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kwamba atapata uzoefu wa kutosha barani Ulaya kama akienda mapema. Wachezaji wa Barcelona ambao ni raia wa Brazil, Dani Alves na Adriano wamekuwa wakimshauri nyota huyo kufanya uamuzi sahihi kwa kujiunga na klabu hiyo hivyo kuongeza chachu ya nyota kumwaga wino hapo. Neymar ambaye atakuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika Juni mwaka huu atasafiri kwenda Hispania muda mfupi baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ili kuzungumzia mustabali wake.

FUFA KATIKA MCHAKATO WA KOCHA MPYA
SHIRIKISHO la Soka nchini Uganda-FUFA limesema kuwa lina uhakika wa timu ya taifa ya nchi hiyo kupata kocha mpya kabla ya mechi zao mbili za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Liberia na Angola zitakazochezwa Juni mwaka huu. Nafasi ya kocha wa nchi hiyo maarufu kama The Cranes ilibakia wazi baada ya Bobby Williamson kutimuliwa wiki iliyopita. Ofisa Habari wa FUFA amesema ni matumaini yao kocha mpya atapatikana kabla ya mechi yao dhidi ya Liberia na anaamini hilo litatokea. Makocha mbalimbali wametuma maombi yao ya kutaka kibarua cha kuinoa The Cranes wakiwemo Dario Bonetti wa Italia, Nikola Kavazovic wa Serbia na Tom Sainfeit wa Ubelgiji ambaye pia amewahi kuinoa Yanga ya Dar es Salaam.

MICHO ASEMA RWANDA ITABAKI MAISHANI MWANGU"
ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ametanabaisha kuwa Rwanda  itabakia kuwa sehemu muhimu katika maisha yake pamoja na kutimuliwa kibarua chake jana. Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Ferwafa jana lilitangaza kukatisha mkataba na kocha huyo kutokana na matokeo yasiyo yakuridhisha ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata. Hivi sasa Micho mwenye umri wa miaka 43 ambaye mkataba wake ulikuwa umelizike Octoba mwaka huu anafanya kazi na washauri wake wa kisheria pamoja na Ferwafa kuangalia jinsi ya kulipwa stahiki zake. Lakini Micho alisisitiza kuwa pamoja na kutoa hayo lakini soka la nchi hiyo wananchi wake pamoja na watu wote aliofanya nao kazi watabakia sehemu muhimu katika maisha akiwa hapo kuanzia mwaka 2011 alipochukua mikoba ya Sellas Tetteh.
WANANDINGA WA KIAFRIKA KATIKA SOKO LA ULAYA

Wachezaji wa Kiafrika wazidi kupata soko Barani Ulaya hivyo Watanzania wasichezee fursa ya soka la kimataifa.
v  Zaidi ya Mawakala 15 wawasiliana na Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji 
 Zaidi ya mawakala 15 tayari wamewasiliana na Kampuni ya Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji mbalimbali kwaajili ya kuwapeleka kwenye klabu za barani Ulaya, Asia na Afrika ili kucheza soka la kulipwa.

Mwitikio huo umeongezeka kutokana na vijana wa kiafrika kuwa na soko kubwa katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu kwa nchi mbalimbali kama Sweden, Uholanzi, Denmark, Ureno na nchi nyinginezo.

Arne Anderson kutoka AA Football Service ya Sweden amesema kuwa binafsi yuko tayari kuchukua wachezaji wawili kwaajili ya kuwatafutia clubs nchini humo kwani tayari mafanikio ya wachezaji watano wa kiafrika aliowapeleka yamempa maombi ya timu nyingi za Sweden.

“Niko tayari kuchukua wachezaji wawili endapo tutakubaliana kuhusu maslahi yangu pindi wachezaji hao wakianza kucheza hapa”, Arne amesema.

Kutokana na mafanikio hayo na maombi ya mawakala lukuki Kampuni ya Tanzania Mwandi inazidi kuwasisitizia wachezaji wa Kitanzania kujaza fomu zinazopatikana kupitia blog.tanzaniamwandi.co.tz ili kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Sweden, Norway, Denmark, Uholanzi, Ureno, Uswiss, Ufaransa na Ubelgiji, barani Asia (Kuwait, China, Qatar nk) na klabu nyingine barani Afrika.

Mpaka sasa jumla ya wachezaji wa kitanzania 15 wamekwishajaza fomu za haraka kwenye tovuti ya Tanzania Mwandi huku kampuni ikiwa imepokea pia maombi ya wachezaji 25 kutoka nje ya nchi.

“Maombi yanazidi kuja ingawa tunawahimiza Watanzania wasikimbie kiingilio cha shilingi 300, 000 wakumbuke kuwa wanafanya majaribio wakiwa nyumbani na watakapopata timu Kampuni ya Tanzania Mwandi haitachukua chochote kwenye mikataba yao, ni wao na mawakala ndio watakokubaliana juu ya watakachokipata kutoka kwa klabu husika”, alisema Teonas Aswile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, waandaaji wa African Youth Football Tournament.

Aswile amezialika klabu mbalimbali za ligi kuu ya soka Tanzania Bara na Visiwani kutazama wachezaji watakaofika katika michuano hiyo kwani wapo baadhi ya wachezaji kutoka nje ya nchi ambao watafika na wangependa kucheza soka la Tanzania.

“Kati ya wachezaji 25 wa nje ya nchi wengine wameomba tuwatafutie timu hapa nchini hivyo klabu zikija zinaweza kuwapata wachezaji hao wakiwa huru kwasababu watakuja kwa gharama zao kufanya majaribio nchini. Pia klabu hizo zitumie fursa hii kuuza wachezaji wake.”
Michuano ya African Youth Football Tournament inatarajia kufanyika Juni 10 hadi 14 mwaka huu katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kati ya miaka 18 hadi 21 kutoka Tanzania na bara zima la Afrika. Taarifa zaidi kuhusu michuano hiyo zinapatikana kupitia;  blog.tanzaniamwandi.co.tz  
Imetolewa na Idara ya Habari
Kampuni ya Tanzania Mwandi,
TANCOT House, Ground Floor,
S. L. P 79944,
Dar es Salaam.
MECHI YA MGAMBO, YANGA YAINGIZA MIL 24/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mgambo Shooting na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 17 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga imeingiza sh. 24,865,000 kutokana na watazamaji 4,386.

Viingilio katika mechi hiyo namba 162 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 vilikuwa sh. 10,000 kwa jukwaa kuu na sh. 5,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 5,547,337.50 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,792,966.10.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 2,820,680.08, msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 90,000, waamuzi sh. 270,000, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 1,587,500.

Mgawo mwingine ni gharama za mechi sh. 1,692,408.05, Kamati ya Ligi sh. 1,692,408.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 846,204.05 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) sh. 658,158.69.

MAKOCHA AZAM, FAR RABAT KUTETA
Makocha wa timu za Azam, Stewart John Hall na AS FAR Rabat ya Morocco, Abderazzak Khairi watakutana na waandishi wa habari kesho (Aprili 19 mwaka huu) kuzungumzia mechi yao itakayofanyika Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkutano huo ambao pia utawahusisha manahodha wa timu hizo mbili utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Barabara ya Uhuru na Shaurimoyo.

Timu hizo zitakutana katika mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho itakayoanza saa 10 kamili jioni. Mechi ya marudiano itachezwa nchini Morocco wiki mbili baadaye.

JKT RUVU, YANGA KUUMANA JUMAPILI
Yanga ambayo inafukuzia kwa karibu taji la Ligi Kuu ya Vodacom itapambana na JKT Ruvu katika mechi pekee ya ligi hiyo wikiendi hii itakayofanyika Jumapili (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbali ya mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa mwezi huu ni kati ya African Lyon na JKT Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nayo Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja wa Taifa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Simba na Polisi Morogoro itakayofanyika Aprili 28.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAMBO YA NDONDI - CHALINZE
WANANDONDI Mwaite Juma,Cosmas Kibuga na Shabani Kaoneka ni baadhi ya mabondia wa Dar es salaam watakaokwenda Chalinze kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa Chalize.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia chipukizi ya Bigright Promotion, imeandaa pambano hilo ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimichezo ikiwemo wilaya ya Chalinze.

Tumeamua kuifanyia Chalinze kwa sababu tunataka iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa Dar na wakali wa Chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu.
ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda kushangilia na kurudi.

wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wa ngumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo
LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA

MSIMAMO:

NA
TIMU
p
W
D
L
GD
PTS
1 
YANGA 
23
16
5
2
28
53
2
Azam FC
23
14
5
4
22
47
3
Kagera Sugar
23
10
7
5
7
40
4
Simba
22
9
9
4
11
36
5
Mtibwa Sugar
24
8
9
6
2
36
6
Coastal Union
23
8
8
6
3
33
7
Ruvu Shooting
22
8
6
8
0
30
8
JKT Oljoro
24
7
7
9
-4
28
9
Prisons FC
24
6
8
10
-7
26
10
Mgambo Shooting
23
7
4
12
-7
25
11
Jkt RUVU
23
6
4
11
-15
23
12
Toto african
25
4
10
10
-12
22
13
Police M
23
3
10
10
-10
19
14
African Lyon
23
5
4
14
-19
19

MATOKEO  JANA

Aprili 17, 2013

Mgambo JKT 1-1 Yanga SC

Kagera Sugar 1-0 Toto Africans

Mtibwa Sugar 1-0 JKT Oljoro

MECHI ZILIZOBAKI VPL
Aprili 21, 2013
JKT Ruvu Vs Yanga SC
Aprili 25, 2013
Ruvu Shooting Vs Simba SC
African Lyon Vs JKT Ruvu
Aprili 27, 2013
Coastal Union Vs Azam FC
Aprili 28, 2013
Simba SC Vs Polisi Moro
Mei 1, 2013
Mtibwa Sugar Vs African Lyon
Yanga SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs TZ Prisons
Polisi Moro Vs Kagera Sugar
Ruvu Shooting Vs JKT Oljoro
Mei 8, 2013
Simba SC Vs Mgambo JKT
Mei 11, 2013
Azam FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting
Mei 18, 2013
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
HATARINI KUSHUKA DARAJA:
1.Polisi moro
2.African lyon
3.Toto african
4.Jkt ruvu
KUZIPISHA TIMU ZILIZO PANDA MSIMU UJAO
1.Mbeya city
2.Ashanti united
3.Rhino rangers
WAARABU WAJA NA VITUKO KEDEKEDE


TIMU ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayoikabili Azam kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho imetua jana (Aprili 17 mwaka huu) saa 7.30 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.

Wapinzani hao wa Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, AS FAR Rabat ya Morocco baada ya kuwasili jana Dar es Salaam wameanza na vituko kedekede.
kwanza wamijawa na  wasiwasi tangu wanatua katika dimba la Uwanja wa Ndege na kutoa imani kwa  wapinzani wao, wakikataa mapokezi na mwishowe  kukataa hoteli waliyokodiwa na wenyeji wao, Sapphire Court.
Pamoja na kuambiwa hoteli hiyo imepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na timu zote zilizocheza na Azam katika mashindano hayo, zilifikia hapo, Al Nasir ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers II ya Liberia, lakini wakagoma.
Wenyeji wakawaambia kama hawataki hoteli hiyo watajilipia popote watakapokwenda na Waarabu hao nao wakaonyesha jeuri ya fedha kwa kujipangia New Africa Hotel. Kaazi kweli kweli.
ukitafakari kwa undani zaidi ni moja ya dalili mbaya kwa Waarabu hao kugomea hoteli na visa vyote walivyofanya, hata hivyo ni hatari kwa Azam  katika wakielekea  Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Azam watakwatuana na timu hiyo ya far rabat {Waarabu hao} Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Morocco na mshindi wa jumla ataingia kwenye droo ya kucheza na timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 
Azam FC ilifanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuichalaza magoli 2-1 Barack Young Contollers II ya Liberia.Ilianza kwa kushinda 2-1 mjini Monrovia kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.