Thursday, May 2, 2013

RONALDINHO KATIKA ULIMWENGU WA SOKA

Ronaldinho
Taarifa kuhusu yeye
Full name
Ronaldo de Assis Moreira
Date of birth
21 March 1980 (age 33)
Place of birth
Height
1.83 m (6 ft 0 in)[1]
Playing position
Timu ya sasa
Current club
Number
10
Timu ya ujana
1987–1998
Timu ya wakubwa 
Years
Team
Mechi
(Goli
1998–2001
52
(21)
2001–2003
55
(17)
2003–2008
145
(70)
2008–2010
76
(20)
2011–2012
33
(15)
2012–
32
(9)
Timu ya taifa
1996
6
(2)
1999
5
(3)
2000–2008
27
(18)
1999–
96
(33)

CLUB MATAJI
Grêmio
·         South Cup (1): 1999
·         Rio Grande do Sul State Championship (1): 1999
Paris Saint-Germain
·         UEFA Intertoto Cup (1): 2001
Barcelona
·         La Liga (2): 2004–05, 2005–06
·         Supercopa de España (2): 2005, 2006
·         UEFA Champions League (1): 2005–06
AC Milan
·         Serie A (1): 2010–11
Flamengo
·         Taça Guanabara (1): 2011
·         Taça Rio (1): 2011
·         Campeonato Carioca (1): 2011


TIMU YA TAIFA Brazil

·         Copa América (1): 1999
·         FIFA World Cup (1): 2002
·         FIFA Confederations Cup (1): 2005
·         Superclásico de las Américas (1): 2011
Brazil U23
·         CONMEBOL Men Pre-Olympic Tournament (1): 1999
·         Olympic Bronze Medal (1): 2008
Brazil U17
·         FIFA U-17 World Championship (1): 1997
TUZO BINAFSI
1.Kombe la Shirikisho Golden boy : 1999
2. Kombe la Shirikisho la Golden ball: 1999
3.Rio Grande do Sul Hali michuano ya mfungaji bora: 1999
4. CONMEBOL Wanaume Kabla ya Olimpiki mashindano mfungaji bora: 2000
5. Kombe la Dunia All-Star Team: 2002
6.FIFA miaka 100
7. Balon di’o tuzo (2): 2003-04, 2005-06
8.La Liga Ibero-American Mchezaji wa Mwaka (1): 2004
9. FIFA World Mchezaji wa Mwaka (2): 2004, 2005
10.Ballon d'Or (1): 2005
11. FIFPro World Mchezaji wa Mwaka (2): 2005, 2006
12. UEFA mfungaji bora wa club (1): 2004-05
13. UEFA Club Mchezaji wa Mwaka (1): 2005-06
14.UEFA Timu ya Mwaka (3): 2003-04, 2004-05, 2005-06
15.FIFPro World XI (3): 2004-05, 2005-06, 2006-07
16 Golden mfungaji bora (1): 2009

EUROPA LIGI-NUSU FAINALI: JE LEO CHELSEA KUTINGA FAINALI

[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 5 Usiku, Bongo Taimu]

MARUDIANO
Alhamisi Mei 2
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Benfica v Fenerbahce [0-1]
Chelsea v FC Basel [1-2]
FAINALI
AMSTERDAM ARENA
MEI 15
Benfica/Fenerbahce v Chelsea/FC Basel 
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
FAINALI WATOTO WA BABA MMOJA
RATIBA/MATOKEO:
MARUDIANO
Jumanne Aprili 30
[Kwenye Mabano Jumla Magoli Mechi 2]
Real Madrid 2 Borussia Dortmund 0 [3-4]
Jumatano Mei 1
Barcelona 0 Bayern Munich 3 [0-7]
MAGOLI:
Barcelona 0
Bayern Munich 3
-Arjen Robben Dakika ya 32
-Pique 72 [Kajifunga Mwenyewe]
-Thomas Mueller 76
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.
Borrussia Dortmund v Bayern Munich

MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA TFF


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanza upya mchakato wa uchaguzi baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili. FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili. Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo kuwa suala la Tanzania lilijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya Dharura ya FIFA kilichofanyika tarehe 28 Aprili 2013 na maamuzi yake kutumwa juzi kwa barua iliyosainiwa na KatibuMkuuwa FIFA, Jerome Valcke. Baada ya kupokea barua hiyo, Rais wa TFF alifunga safari kwenda Dodoma jana kukutana na Mheshimiwa Waziri na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT). “Matarajio yetu sote yalikuwa kupokea majina ya waliopitishwa ili tufanye uchaguzi. Kinyume chake tumepokea maagizo hayo. Hata hivyo tumeona kuwa hili ni jambo la kheri kwa vile siyo tu haki itatendeka bali pia itaonekana imetendeka.” alisema Tenga, ambaye alishatangaza kuwa hatagombea tena urais baada ya kuliongoza Shirikisho kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja. “Lengo letu ni kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa na uchaguzi kufanyika mapema iwezekanvyo kabla ya tarehe iliyotolewa. Yale mambo nayoweza kufanyika kwa pamoja yatafanyika ili tuharakishe utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na FIFA." Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyik tarehe 23 na 24 Februari 2013 na ulikuwa ukielekea ukingoni, lakini baadhi ya wagombea walienguliwa katika hatua ya mwisho na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na ndipo walipo andika barua FIFA kuomba iingilie kati. Rais Tenga alisema kuwa ujumbe wa FIFA ulikutana na pande zote zilizoathiriwa na mchakato wa uchaguzi na kwamba baada ya kukusanya taarifa hizo, maagizohayo ya FIFA sasa yatakuwa ni suluhisho la matatizo ya muda mrefu katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

Katika barua hiyo, FIFA imeiagizaTFF:

1. Kuunda vyombo sahihi (Kamati ya Maadili itakayokuwa na vyombo viwili ambavyo ni cha kutoa maamuzi ya awali na cha rufaa) ambavyo mamlaka yake yatakuwa ni kushughulikia masuala ya ukiukwaji wa maadili;

2. Kufanya mabadiliko ya katiba kwa kuzingatia uundwaji wa vyombo hivyo;

3. Kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Utendaji kwa kufungua milango kwa wagombea ambao walishachukua fomu na wagombea wapya:
4. Shughuli hiyo ikamilike ifikapo tarehe 30 Oktoba 2013.
Katika kutekeleza hayo, TFF inatakiwa iitishe Mkutano Mkuu wa Dharura kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kuunda kamati hizo za maadili na Kanuni za Uchaguzi kabla ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati Mpya ya Utendaji.
Katika maoni yake FIFA imeeleza kuwa katika mchakato, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua au kupitisha baadhi ya wagombea kwa kubaini kuwa walikiuka Ibara ya 9 (7) ya Kanuni za Uchaguzi na pia Ibaray a 29 (7) ya Katiba ya TFF ambavyo vinahusisha suala la kufungua kesi mahakamani, kufuja fedha za shirikisho na ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja.
Hata hivyo, FIFA ilisema kuwa watu hao walitakiwa waadhibiwe kwanza na kamati husika (kamati za maadili) kabla ya kuenguliwa na kamati za uchaguzi za TFF.

Kutokana na ukosefu wa kamati za maadili matokeo yake, mmoja wa wagombea amekuwa akienguliwa kwenye uchaguzi kila anapombea bila ya kujua adhabu yake ni ya muda gani,” inasema barua hiyo ya FIFA.

Rais Tenga ameagiza kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kupokea maagizo ya FIFA na kupanga ratiba ya utekelezaji wake kwa lengo la kuhakikisha kuwa mchakato huu unatekelezwa mapema iwezekanavyo.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 1, 2013
 MIKOA 18 YAPATA MABINGWA WA MIKOA
Mikoa 18 kati ya 27 ya kimpira tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu tatu za juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014). Ligi ya FDL ina jumla ya timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu ni Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa na Morani FC ya Manyara.

Mabingwa waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).

Wengine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).

Kila klabu inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.

MTANZANIA AOMBEWA ITC ACHEZE NORWAY
Shirikisho la Mpira wa Miguu Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili aweze kucheza mpira nchini humo.

NFF inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini Norway.

AZAM YAENDELEA KUJINOA MOROCCO
Timu ya Azam ambayo iko jijini Rabat kwa ajili ya mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabati ya huko inaendelea vizuri na mazoezi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi wa Azam FC, Jaffer Idd maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Mei 4 mwaka huu). Jaffer Idd anapatikana kwa namba +212671146092.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, April 30, 2013

LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA DIMBANI KESHO YANGA USO KWA USO NA WAGOSI


.

LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA 25
 Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi. Licha ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013), mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu nchini. Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa. Viingilio katik mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo. Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons. Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.

MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji. Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo. Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji. 

MECHI YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/- Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000. Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.

Monday, April 29, 2013

AZAM FC WATUA MOROCO KWA MCHEZO WA MARUDIANO


CLUB ya  azam FC imefika salama nchini Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji, FAR Rabat, Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii.  

Azam, imewasili Cassablanca, majira ya saa 9:15 za huku Alasiri, sawa na saa 10:15 za Afrika Mashariki na kusafiri kwa basi kwa saa mbili kwenda Rabat, mji ambao mechi itachezwa.

Azam imetua Morocco ikitokea Dubai, UAE ambako ilifika usiku jana saa 6:00 kwa saa za huko sawa na saa 5:00 kwa saa za Afrika Mashariki, ikitokea Dar es Salaam.
Msafara huo unaouhusisha wachezaji na benchi la Ufundi, baada ya awali viongozi na wapenzi kadhaa kutangulia nchini humo, ili kuweka mazingira sawa, uliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la Emirates, wadhamini wa Arsenal ya England saa 11:00 jioni kwa saa za Tanzania.
Ni safari ndefu iliyohusisha mabara mawili, kutoka Afrika, Tanzania kupitia Asia Dubai na kurudi Afrika nchini Morocco.
Azam walilala katika hoteli ya nyota tano ya Copthorne Dubai kabla ya kuunganisha ndege saa 7:35 asubuhi ya leo kuja Morocco kesho.
Azam imefikia katika hoteli ya Golden Tulip, maeneo ya Rabat, kaskazini mwa Cassablanca,  kilomita 120 kutoka Uwanja wa Ndege wa Cassablanca, umbali wa takriban saaa mbili.

Azam itaanza rasmi mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo, ambao wanatakiwa kutoa sare ya mabao au kushinda ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita.
Azam, itakuwa Rabat kwa wiki nzima hadi Jumamosi itakapocheza mechi na imejipanga vema kuhakikisha inavuka hatua hii. 

DIMBANI UCL-NUSU FAINALI KUENDELEA LEO

MARUDIANO
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund [1-4]
Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich [0-4]
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.

MECHI ZILIZOBAKI KWA KUTAFUTA 4 BORA LIGI KUU UINGEREZA BPL
ARSENAL-Mechi zilizobaki:
4 Mei: QPR [Ugenini]
14 Mei: Wigan [Nyumbani]
19 Mei: Newcastle [Ugenini]
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
CHELSEA-Mechi zilizobaki:
5 Mei: Man United [Ugenini]
8 Mei: Tottenham [Nyumbani]
11 Mei: Aston Villa [Ugenini]
19 Mei: Everton [Nyumbani]
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
TOTTENHAM-Mechi zilizobaki:
4 Mei: Southampton [Nyumbani]
8 Mei: Chelsea [Ugenini]
12 Mei: Stoke [Ugenini]
19 Mei: Sunderland [Nyumbani] 

MSIMAMO
NA TIMU P GD PTS
1 Man Utd 35 43 85
2 Man City 34 30 71
3 Chelsea 34 33 65
4 Arsenal 35 30 64
5 Tottenham 34 17 62
6 Everton 35 14 59
7 Liverpool 35 25 54