Wednesday, June 19, 2013

BENZEMA VS RIBERY KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA NGONO"

Wanandinga wa Kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery na Karim Benzema wamefikishwa mahakamani leo jijini Paris wakituhumiwa kutembea na mwanamke anayejiuza mwenye umri mdogo. Ribery ambaye anacheza katika klabu ya Bayern Munich na Benzema anayekipiga katika klabu ya Real Madrid watakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini inayozidi euro 45,000 kama wakikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo. Nyota hao wote wawili walikana tuhuma hizo huku mwanamke huyo aitwaye Zahia Dehar alitoa ushahidi kuwa wote wawili hawakuwa wakijua kama hajafikisha umri huo wakati wakifanya naye mapenzi mwaka 2008 na 2009. Pamoja na kwamba umri halali ni miaka 15 nchini Ufaransa lakini kumlipa mwanamke anayejiuza chini ya umri wa miaka 18 ni kosa.

Tuesday, June 18, 2013

MAKALA KUHUSU UCHAMBUZI WA TAIFA STARS""


TAIFA Stars timu ya soka ya Taifa ya Tanzania,imefanikiwa kulala ikiwa nyumbani baada ya kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory Coast na kuzima harakati za hapa na pale za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil.
Amini watanzania wengi na wadau wa michezo nchini waliweka matumaini na kudhani Taifa Stars ingeweza kusonga mbele katika harakati hizo za kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014, lakini sasa ukweli kila kitu kipo wazi na ukweli umejionyesha.
Asilimia  kubwa ya watanzania Sasa wamekubaliana na uhalisia wa mambo kwamba Timu ya Taifa ifike tunako taka inahitaji muda kidogo kuona Taifa Stars ikisonga mbele katika kuelekea kufuzu Kombe la Dunia na siyo rahisi kama ilivyodhaniwa hapo kabla.
Ni mambo mengi yaliyotokea katika mchezo dhidi ya Ivory Coast ambayo yaliigharimu Taifa Stars licha ya uwanja kujaa idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wakiishangilia timu yao bila kuchoka.
Jambo la msingi ni kwamba, Taifa Stars ikiwa katika harakati za kuhakikisha inafuzu Kombe la Dunia wengi tulisahau kwamba kiukweli ilikuwa ngumu kwa Taifa Stars kufuzu fainali hizo japokuwa kwa mapenzi tulidhani timu hii ingeweza kufuzu kwa kuanza na vipigo kwa timu za Morocco na Ivory Coast.
Tukitazama mchezo kati ya Taifa Stars na Ivory Coast kuna baadhi ya mambo yalionekana kwamba bado tuna safari ndefu ya kufuzu Kombe la Dunia kama kweli tuna nia ya kufanya hivyo.
Mambo mengi mno yalijitokeza katika mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast na haya ni machache kati ya mengi yake.
1.Umakini wa safu ya ulinzi ulikuwa hafifu -katika kudhibiti kasi ya Salomon Kalou pamoja na Gevinho walikuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya tanzania.
"Natumai hapa mdau wa mtandao huu utafahamu kabisa nini ambacho namaanisha safu ya ulinzi wachezaji wakucheza katika nafasi zao.
Hapa katika hali ya kawaida ilionekana upande wa mchezaji Erasto Nyoni unaweza kubeba lawama nzito lakini halikuwa kosa lake kwani alilazimika kwenda katikati kuongeza nguvu na kusawazisha makosa ya mabeki wa kati ambapo ilipelekea kusahau nafasi yake na majukumu aliyopewa.
Katika hali ya kawaida kiukweli ilionekana‘njia’ tangu dakika za mwanzo, beki Erasto Nyoni inaonekana hakupata ushauri wa kutosha kuhusu kutulia na kucheza soka kwani hata makelele ya mashabiki yalimfanya aonekane mtu asiyefa hatuweza kumlaumu.
2.Nguvu ndogo ya wachezaji wa Taifa Star- 
Safu ya kiungo- kwa upande wa Ivory Coast ikisimamiwa vilivyo na Yaya Toure  licha ya mchezo wa jana kucheza safu ya ushambuliaji aliweza kutimiza majukumu aliyopewa na kocha wake kiukweli kiungo huyu wa Club ya Man city alionyesha uwezo wake na kuwazidi wachezaji wa Taifa Star Abubakar Sure boy ambaye ni mfupi na mwenye umbo dogo alionekana mchezaji wa kawaida mbele ya Yaya Toure ambapo pia Frank domayo pamoja na Mwinyi Kazimoto licha ya kucheza vizuri lakini maumbo yao walionekana kutoweza kuhimili mikimikiya Traore Lucina na Jean Jacques ambao wote ni watu wenye miili mikubwa pia hilo lilikuwa moja ya jambo lililoigharimu timu. 
3.Ubora wa wachezaji wa Ivory Coast-Kila mtu anafahamu Kabisa kuwa kikosi cha Timu ya hiyo kinawachezaji wengi wenye uzoefu wanaocheza katika ligi mbalimbali Barani ulaya wemeonekana kujiamini mbele ya wachezaji wa Taif Star na kujipa Matumaini kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo ule. kwa ufupi tu kwa haraka haraka kila mdau wa michezo anafahamu uwezo wa Yaya Toure,Solomon Kalou,Gervinho na wengineo kina Bakari Kone nk.

4.Umakini Mbovu wa Safu ya Ushambuliaji- Licha ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu Mbwana Samata ,Tomas Ulimwengu pamoja na Amri Kiemba kwa kushirikiana kwa pamoja na kuweza kupata Mabao Mawili" Hapa wachezaji hawa walionekana kutopeana nafasi na kujipanga vizuri kuhakikisha wanajipatia nafasi nzuri za kutupia mabao wavuni.
5.Mbali ya yote'' Taifa star inastahili pongezi kwa kuweza kumiliki mpira na kuonyesha kandanda safi katika mchezo huo hivyo kubwa zaidi watanzania tuamini kabisa katika michuano ya CHAN inayo kuja lazima tutashiriki kutokana na ubora wa kocha wetu Kim Poulsen ambaye kiukweli ameweza kuitengeneza timu kucheza kwa kujiamini licha ya kupoteza mchezo ule" Hivyo kubwa zaidi ni kuipa Support Timu yetu ya Taifa. Ahsanteni.

PONGEZI KWA WASHABIKI KUIUNGA MKONO STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2.
Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
 RWIZA KUHUDHURIA SEMINA YA MAKAMISHNA CAF
Kamishna Alfred Kishongole Rwiza ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhudhuria semina ya makamishna itakayofanyika kuanzia Julai 6-7 mwaka huu katika makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri.
Semina hiyo inashirikisha baadhi ya makamishna wa CAF walioko kwenye orodha ya makamishna ya shirikisho hilo kwa mwaka 2012-2014.
Rwiza ni mmoja wa makamishna wa CAF kutoka Tanzania, na mechi ya mwisho kusimamia ilikuwa ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Mei mwaka huu nchini  Msumbiji.
CAF tayari imeshamtumia tiketi Rwiza, na anatarajia kuondoka nchini Julai 4 mwaka huu kwenda Cairo kwa ndege ya EgyptAir.
 MTANZANIA APEWA ITC ACHEZE YEMEN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Gossage Mtumwa ili aweze kucheza mpira nchini Yemen.
 Mtumwa ambaye anatoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji cha Rollingstone cha Arusha aliombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Yemen (YFA) kwa ajili ya kucheza nchini humo.
 TFF inamtakia kila la kheri Mtumwa katika safari yake ya Yemen, na ni matarajio yetu kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania nchini humo ili wachezaji wengine wa Tanzania nao wapate fursa ya kucheza mpira wa miguu nchini Yemen.
 KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA
Klabu ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.
Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.
Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).
 Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).
 Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Monday, June 17, 2013

KOMBE LA MABARA NCHINI BRAZIL HISPAIN YAILAZA URUGUAY

Katika mechi ya kwanza ya ufunguzi  wa Michuano ya FIFa Kombe la Mabara inayochezwa huko nchini Brazil ambapo katika Kundi B mabingwa wa dunia Timu ya Taifa ya Hispain imefanikiwa kuibamiza Uruguay goli 2-1 kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Arena Pernambucho Mjini Recife.
Goli za hispain zilitiwa kimiani na pedro na Robert Soldado katika dakika za 20 na 32 huku bao la kufutia machozi kwa Uruguay imefungwa na mshambuliaji nyota wa Club ya Liverpool Luis Suarez dakika ya 88 ya mtanange huo huku Hispain ikitawala kwa kiwango cha juu.
Kwa upande wake Kocha wa Hisapin Vicent del bosque ametanabaisha kuwa ushindi huo wa mechi ya kwanza umewapa point 3 muhimu na kukiri walichoka katika kipindi cha mwisho kutoka na hali ya hewa ya joto.
MSIMAMO KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Spain
1
 1
0
0
 2
 1
 1
 3
2
Uruguay
1
 1
0
1
 1
 2
-1
 0
3
Nigeria
0
 0
0
0
 0
 0
  0
 0
4
Tahiti
0
 0
0
0
 0
 0
  0
 0

MSIMAMO KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Brazil
1
 1
0
0
  3
 0
  3
 3
2
Italy
1
 1
0
1
  2
 1
  1
 3
3
Mexico
1
 0
0
1
 1
 2
 -1
 0
4
Japan
1
 0
0
1
 0
   3
  -3
 0
 Juni 15
Brazil 3 Japan 0
Juni 16
Mexico 1 Italy 2
Saa 7 Usiku
Hispain 2 Uruguay 1
Saa 4 Usiku
RATIBA MECHI YA LEO JUNI 17
Tahiti vs Nigeria
Saa 4 Usiku
Uwanja – {Belo Holizonte}
JUMA TANO JUNI 19
Brazil vs Mexico
Saa 4 Usiku
Uwanja-{Fortaleza}
Italy vs Japan
Saa 7 Usiku
Uwanja- {Recife}

Sunday, June 16, 2013

JUPP HEYNCKES AWEKA WAZI KUTOFANYA KAZI YA UKOCHA

Baada ya kuipa mafanikio ya kutosha Bayern muninch Jupp Heynckes hatimaye amebainisha kuwa hataendelea kufanya kazi hiyo baada ya kuondoka kwa mabingwa wa soka barani Ulaya. Bayern wakiwa chini ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 wamefanikiwa kumaliza msimu kwa mafanikio kwa kunyakuwa mataji matatu ya Bundesliga, DFB-Pokal na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mafanikio hayo Bayern imekuwa klabu ya saba barani Ulaya kufanikiwa kushinda mataji matatu mfululizo. Hatahivyo Heynckes ameamua kustaafu kufundisha baada ya nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola.

FIFA YATANGAZA KUWA MZUNGUUKO WA TATU KUFUZU KOMBE LA DUNIA NI MWEZI SEPTEMBER.

SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limetangaza kuwa mzunguko wa tatu wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 pamoja na hatua ya mtoano kwa nchi za barani Ulaya itafanyika Septemba na Octoba mwaka huu. Ratiba kwa upande wa nchi za Afrika ambazo zitajumuisha washindi kutoka katika makundi 10 itafanyika Septemba 16 jijini Cairo, Misri ambapo nchini tano zilizo juu katika viwango vya ubora vya FIFA ndizo zitaongoza ratiba hiyo. Nchi nane zitakazomaliza katika nafasi ya pili barani Ulaya nazo zitapangiwa ratiba jijini Zurich, Switzerland Octoba 21 huku nchi nne kati ya zilizo juu katika viwango vya FIFA zikiongoza ratiba hiyo. Tanzania inajitupa uwanjani leo kuvukuzia nafasi ya kuingia katika ratiba hiyo kwa kupambana na Tembo wa Ivory Coast katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.