Saturday, April 5, 2014

SIMBA YABANWA NA KAGERA,HUKU MBEYA CITY IKIVUTWA SHATI NA ASHANTI

MATOKEO
Jumamosi Aprili 5
Kagera Sugar 1 Simba 1
Ashanti United 0 Mbeya City 0
Katika Michezo miwiili pekee iliyopigwa ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, zilizochezwa LEO, Kagera Sugar na Simba zilitoka Sare ya Bao 1-1 huko Kaitaba, Mjini Bukoba na huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Ashanti United ilitoka 0-0 na Mbeya City.
Huko Kaitaba, Simba walitangulia kufunga katika Dakika ya 45 kwa Bao la Zahor Pazi na Kagera Sugar kusawazisha Dakika ya 51 kwa Bao la Themi Felix.
Ligi itaendelea hapo kesho na zipo Mechi 4 ikiwemo ile ya Yanga v JKT Ruvu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

VPL: LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumapili Aprili 6
Coastal Union v Mgambo JKT
JKT Oljoro v Tanzania Prisons
Rhino Rangers v Mtibwa Sugar
Yanga v JKT Ruvu
Jumatano Aprili 9
Ruvu Shooting v Azam FC
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
23
15
8
0
31
53
2
Yanga SC
22
13
7
2
26
46
3
Mbeya City
24
12
10
2
13
46
4
Simba SC
24
9
10
5
15
37
5
Kagera Sugar
23
8
10
5
3
34
6
Mtibwa Sugar
22
7
8
7
1
29
7
Coastal Union
23
6
11
6
0
29
8
Ruvu Shooting
21
7
8
6
-4
29
9
JKT Ruvu
23
9
1
13
-13
28
10
Ashanti United
23
5
7
11
-17
22
11
Mgambo JKT
22
5
6
11
-18
21
12
Prisons FC
22
3
10
9
-10
19
13
JKT Oljoro
23
2
9
12
-18
15
14
Rhino Rangers
23
2
7
14
-19
13

TAIFA STARS, BURUNDI KUCHEZA APRILI 26

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki na Burundi (Intamba Mu Rugamba) Aprili 26 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa ajili ya mechi hiyo ikiwa na wachezaji waliopatikana katika programu maalumu ya kusaka vipaji.
Baadaye wachezaji wengine wa Taifa Stars ambao wapo nje ya programu ya kusaka vipaji wataungana na wenzao kabla ya kutengeneza kikosi cha mwisho kitakachoivaa Burundi.
Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachezeshwa na waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka nchini Kenya.
TIMU YA WATOTO WA MITAANI YACHACHAFYA BRAZIL
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia yanayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil baada ya jana kuifunga Indonesia kwa jumla ya mabao 5-3.
STREET_CHILD
Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo unamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2 ndipo ikatumia mikwaju ya penalti kuamua mshindi. Tanzania ilipata penalti tatu dhidi ya moja ya wapinzani wao.
Kwa matokeo hayo, Tanzania sasa itacheza mechi ya nusu fainali leo dhidi ya Marekani ili kupata timu zitakazocheza mechi za fainali na kutafuta mshindi wa tatu. Mechi za fainali na kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho (Aprili 6 mwaka huu).
Timu nyingine zilizoingia nusu fainali na mechi zake zinachezwa leo (Aprili 5 mwaka huu) ni Burundi itakayocheza na Pakistan.
Katika mechi zilizopita, Tanzania ilitoka sare ya mabao 2-2 na Burundi, ikaitandika Argentina mabao 3-0 ikailaza Nicaragua mabao 2-0 na ikafungwa na Philippines mabao 2-0.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Friday, April 4, 2014

WAZEE WA JANGWANI YAMKATIA RUFAA MCHEZAJI WA JKT MGAMBO.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara yanga sc imekata rufaa dhidi ya mchezaji Mohammed Neto wa Mgambo Shooting ikidai anacheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kinyume cha kanuni za usajili.
Yanga SC wanalalamikia usajili wa mchezaji huyo una mapungufu kwa kuwa ni raia wa kigeni, lakini hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Evodius Mtawala amekiri kupokea rufaa ya Yanga SC, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi. “Ndiyo tumepokea, ila nipo kwenye kikao siwezi kuzungumza zaidi,”alisema Mtawala, anayekaimu nafasi ya Celestine Mwesigwa aliye Afrika Kusini kwa sasa.
Dhamira ya Yanga SC kutaka rufaa hiyo inaweza kuwa kukomboa pointi walizopoteza kwa Mgambo JKT Jumapili iliyopita kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu.
Lakini kwa mujibu wa kanuni za sasa za Ligi Kuu, baada ya usajili hutolewa muda maalum wa pingamizi kwa wachezaji na anapopitishwa hata ikikatwa rufaa, haibadili matokeo zaidi mchezaji au kiongozi aliyefanya udanganyifu kuchukuliwa hatua.
Lakini pia katika utaratibu wa sasa wa usajili, kila mchezaji mpya katika Ligi Kuu anatakiwa kuwasilisha ama cheti cha kuzaliwa au hati ya kusafiria- ambavyo pamoja na kusaidia umri wa mchezaji kujulikana pia huainisha uraia wake.
Neto alicheza kwa dakika 30 tu mechi dhidi ya Yanga baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Alipewa kakadi ya njano ya kwanza akikataa kukaguliwa na refa Alex Mahagi na ya pili kwa kuzozana na refa huyo akipinga kusachiwa kama amebeba hirizi.
Yanga SC inahaha kuhakikisha inafufua matumaini ya kutetea ubingwa wake na sasa inahamishia nguvu zake mezani, baada ya mambo kuwaendea kombo uwanjani na kuachwa na Azam FC katika mbio hizo.
Azam FC inaongoza kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23 ni ya tatu.