Saturday, May 4, 2013

RAIS WA ZAMANI WA BARKA AFUNGUKA KUHUSU VILANOVA

RAIS wa zamani wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta anaamini kuwa klabu hiyo ilifanya uamuzi usiokuwa sahihi kumteua Tito Vilanova kama kocha mkuu mwanzoni mwa msimu wa 2012-2013. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alitajwa kuchukua nafasi ya Pep Guardiola na kupewa mkataba wa mwaka mmoja lakini Laporta anafikiri Vilanova hakuwa tayari kwa nafasi hiyo kwa kipindi kile. Laporta amesema walimteua Vilanova kwasababu walikuwa wanaogopa kuwa nani ataweza kuchukua nafasi ya Guardiola lakini ilikuwa mapema sana kufanya uamuzi huo. Laporta aliendelea kusema kuwa Barcelona walipaswa kutafuta mbadala wa kocha mwingine wakati Vilanova alipokuwa ameondoka kwa matibabu ya kansa nchini Marekani ingawa alikiri ungekuwa uamuzi mgumu kufanya hivyo ila kulikuwa hakuna jinsi.

COSAFA CUP 2013: KUANZA KUTIMUA VUMBI JULAI 6 TAIFA KATIKA MAKUNDI


Kwa mujibu wa Listi ya Ubora ya FIFA iliyotolewa Aprili 11 mwaka huu Waandaaji wa michuano hii  ndio imetumika kuamua Nchi zipi zitaanzia hatua ya Makundi na zipi zitaanza kucheza hatua ya Raundi ya Mtoano ya Robo Fainali.

Kulingana na mfumo wa Mashindano haya, Timu ambazo zitafungwa Robo Fainali nazo zitasonga kwenye Nusu Fainali yao maalum hadi Fainali yao na Mshindi wake atatwaa Ngao.
hivyo Washindi wa Robo Fainali watasonga na Bingwa kwenye Fainali ndie atatwaa Kombe rasmi la 2013 COSAFA CASTLE CUP.

RATIBA:HATUA YA MAKUNDI
6 JULAI 2013
14:30 Tanzania v Mauritius Nkoloma Stadium, Lusaka
17:00 Namibia v  Seychelles Nkoloma Stadium, Lusaka
8 JULAI 2013
14:30 Mauritius v Namibia Nkoloma Stadium, Lusaka
17:00 Tanzania v Seychelles Nkoloma Stadium, Lusaka
10 JULAI 2013
15:00 Tanzania v Namibia Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
15:00 Mauritius v Seychelles Nkoloma Stadium, Lusaka
KUNDI B:
-Kenya
-Botswana
-Lesotho
-Swaziland
RATIBA:
7 JULAI 2013
13:00 Kenya v Lesotho Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
15:30 Botswana v Swaziland Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
9 JULAI 2013
13:00 Lesotho v Botswana Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
15:30 Kenya v Swaziland Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
11 JULAI 2013
15:00 Kenya v Botswana Nkoloma Stadium, Lusaka
15:00 Lesotho v Swaziland Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
RAUNDI YA MTOANO:
HATUA YA ROBO FAINALI:
13 JULAI 2013
13:00 Zimbabwe v Malawi Nkoloma Stadium, Lusaka
15:30 South Africa v Group A winner Nkoloma Stadium, Lusaka
14 JULAI 2013
13:00 Angola v Group B winner Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
15:30 Zambia v Mozambique Godfrey 'Ucar' Chitalu 107 Stadium, Kabwe
TAZAMA TIMU HIZI KATIKA LISTI  YA UBORA FIFA
*Zambia 45
*South Africa 62
*Angola 94
*Zimbabwe 101
*Mozambique 106
*Malawi 109
*Tanzania 116
*Kenya 122
*Botswana  22
*Namibia 125
*Lesotho 156
*Swaziland 183
*Mauritius 189
*Seychelles 199

AZAM FC NJE KATIKA MICHUANO YA CAF KWA BAO 2-1


Timu ya  Azam FC ya Tanzania imetolewa rasmi  katika Michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa Bao 2-1 na FAR Rabat katika Mechi ya Marudiano iliyochezwa Uwanja wa Complexe Sportif Moulay Abdallah, Jijini Rabat Nchini Morocco.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Wiki mbili zilizopita Timu hizi zilitoka sare ya 0-0.
Nahodha wa Azam, John Bocco, ndie aliefunga bao la kwanza katika Dakika ya 6 na FAR Rabat kusawazisha kwa Penati ya Abderrahim Achakhir na kunako Dakika ya 34 Abderrahim Achakhir huyo huyo alitolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya.
Licha ya kuwa 10 dimbani, FAR Rabat walipata Bao la pili katika Dakika ya 43 mfungaji akiwa Moustapha Allaoui.
Kipindi cha Pili, Azam FC walipata pigo pale katika Dakika ya 55 David Mwantika kupewa Kadi Nyekundu na Nyekundu nyingine kufuatia kwa Wazir Omar katika Dakika ya 74.
Hata hivyo, Azam FC walipata nafasi ya dhahabu katika Dakika ya 82 kwa kupewa Penati lakini John Bocco akakosa kufunga Bao la kusawazisha ambalo lingefanya Mechi iwe 2-2 na Azam kusonga kwa Bao za ugenini.
KIKOSI CHA AZAM:
Mwadini, Himidi, Waziri, Mwantika, Atudo, Bolou, Umony, Salum Abubakar, Bocco, Mieno, Kipre
Akiba: Aishi, Mwaipopo, Mwaikimba, Abdi Kassim, Mcha Viali, Jabir, Luckson
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Mei 3
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Al Ismaily – Egypt 0 FC Ahli Shandi – Sudan 0 [4-3]
Jumamosi Mei 4
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
FAR Rabat – Morocco 2 Azam FC– Tanzania 1 [2-1]
Union Sportive Bitam – Gabon 0 Union Sportive Médina d'Alger – Algeria 3 [0-3]
Supersport United - South Africa 1 Enppi – Egypt 3 [1-3]
Lydia LB Académi – Burundi 2 ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast 0 [2-1]
E.S. Sahel – Tunisia 6 Recreativo Da Caala - Angola 1[7-2]
Jumapili Mei 5
[Kwenye Mabano Matokeo ya Kwanza]
Wydad Athletic Club – Morocco v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique [0-2]Diables Noirs – Congo v Club Sportif Sfaxien – Tunisia [1-3]

Friday, May 3, 2013

SEPP BLLATTER - AWEKA NIA YA KUGOMBEA TENA URAIS WA FIFA

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ametoa dondoo ya kwamba ana mpango wa kugombea tena nafasi hiyo kwa miaka minne mingine wakati wa hotuba yake mara baada ya mkutano na viongozi wa Shirikisho la Soka la Asia-AFC nchini Malaysia. Mapema Machi mwaka huu Blatter amesema ana mpango kwa kuachia ngazi wakati atakapomaliza kipindi chake cha miaka minne kitakapoisha mwaka 2015 lakini akaongeza kuwa ataachia nafasi hiyo pale atakapoamini kwamba atakayemwachia anaweza kulisongesha mbele gurudumu la shirikisho hilo. Blatter mwenye umri wa miaka 77 alirudia tena kauli ya katika mkutano wa AFC jijini Kuala Lumpur jana akidai kuwa yeye ni nahodha na hawezi kuachia meli yake izame wakati bado anaona ana nguvu za kuizuia isifanye hivyo. Kauli hiyo ya Blatter imewafanya wachambuzi wa mambo ya soka wadai kuwa rais huyo ana mpango wa kugombea urais kwa kipindi kingine baada ya kumaliza hiki cha sasa mwaka 2015. Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Michel Platini ambaye alikuwepo katika mkutano huo ambao ulishuhudia Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa wa Bahrain akiteuliwa kuwa rais wa AFC, ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kushika nafasi ya Blatter atakapoacia madaraka. 

BENITEZ AWATAKA MASHABIKI WA CHELSEA KUMUHESHIMU


Rafael Benitez kocha wa muda wa chelsea amesema anastahili kuheshima kwa kuipeleka Chelsea kutinga Fainali ya EUROPA LIGI ambapo watakutana na Benfica huko Amsterdam ArenA hapo Mei 15.








Wakiwa katika dimba la uwanja wa Stamford Bridge katika Mechi ya Marudiano ya
Nusu Fainali ya EUROPA LIGI na FC Basel huku wakiwa wameshinda Bao 2-1
toka Mechi ya kwanza, Chelsea walitanguliwa Bao 1-0 hadi Mapumziko
 lakini Kipindi cha Pili waliisambaratisha Basel kwa kuitandika Bao 3 ndani ya
Dakika 9 kwa Bao za Torres, Moses na Luiz.
MAGOLI:
Chelsea 3
*Torres Dakika ya 50
*Moses 52
*Luiz 59
FC Basel 1
*Salah Dakika ya 45
Hii ni Fainali ya 10 kwenye himaya ya Mmiliki Roman Abramovic huku
 Chelsea wakitwaa  Mataji 11 na watakuwa wakiwania Rekodi ya kuwa
 Klabu ya 4 Barani Ulaya kuweza kutwaa Mataji yote makubwa ya Ulaya
yakiwemo UEFA CUP WINNERS CUP [Kombe la Washindi] na
UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Chelsea, ambao walitwaa Kombe ambalo sasa halipo, Kombe la Washindi,
mara mbili Miaka ya 1970/71 na 1997/98, pamoja na la Klabu Bingwa Ulaya Mwaka jana
, hawajawahi kutwaa UEFA CUP, ambalo sasa ndio EUROPA LIGI.
Klabu nyingine 3 ambazo zimefuzu kutwaa Mataji yote hayo makubwa ni Juventus, Ajax
 na Bayern Munich.
MAKOMBE ENZI ZA ABRAMOVICH:
*BPL 3
*FA CUP 3
*KOMBE LA LIGI 2
*UEFA CHAMPIONZ LIGI 1
*NGAO YA HISANI 2

LIEWIG AFUNGUKA KUHUSU MECHI NA WATANI ZAO WA JADI


Kocha Mkuu wa Wekundu wa msimbazi Simba, Patrick Liewig amesema kuwa silaha yake kubwa katika mechi dhidi ya Yanga  may 18 mwaka huu ni kasi ya wachezajiwake, ingawa amekiri wanatakiwa kuwa makini kwa dakika zote 90 za mchezo.

Mfaransa huyo alisema jijini Dar es Salaam kuwa tayari wamepoteza ubingwa wa ligi pamoja na nafasi ya pili ambayo
ingeweza kuifanya timu hiyo ishiriki Kombe la CAF mwakani.
aidha amesema hakuna  nafasi tena ya kushinda taji la ligi kwa msimu huu wala kumaliza katika nafasi ya pili ambayo ingetupa fursa ya kushiriki Kombe la CAF mwakani.

kubwa zaidi Kilichobaki ni kulinda heshima yetu kwa kuwafunga mabingwa (Yanga) katika mchezo wetu wa mwisho hiyo Mei 18. Timu yangu ya Simba ina wachezaji wengi vijana ambao wana kasi kubwa kuwazidi Yanga." alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic aliyetupiwa virago na klabu hiyo mwaka jana.
Kocha huyo ameongeza na kusema kuwa Yanga ni timu nzuri hakuna mtu anayepinga hilo, lakini haiwezi kumudu kasi ya wachezaji wangu vijana.

hata hivyo liewing amesema Nimewaona katika mechi kadhaa za ligi, wanacheza vizuri ingawa sitaki kuaminikwamba watashinda mbele ya vijana wangu imara."
Liewig amesema katika kambi ya kujiwinda na mchezo huo ataongeza muda wa programu yake ya mazoezi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa katika hali nzuri ya ufiti kabla ya kukutana na watani hao wa jadi katika soka la Tanzania Bara na kuharibu sherehe za ubingwa huo.

25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu uchaguzi wa shirikisho.

Kikao hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa.

FIFA katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe umefanyika kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

KILA LA KHERI AZAM KOMBE LA SHIRIKISHO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayochezwa Morocco kesho (Mei 4 mwaka huu).

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

Azam iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.

25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS
Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.

Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.

KAMATI YA MASHINDANO KUPITIA MAANDALIZI RCL
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyopangwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Tayari mikoa 18 kati ya 27 kimpira imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya RCL itakayotoa timu tatu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014).

Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF itapokea taarifa ya maandalizi ya ligi hiyo kutoka Idara ya Mashindano ya TFF na kufanya uamuzi juu ya mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wao.

Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na ratiba (draw) itapangwa wakati wowote. Ada ya kushiriki ligi hiyo kwa kila klabu ni sh. 100,000 na usajili utakaotumika na ule ule wa ligi ngazi ya mkoa. Hakutakuwa na usajili mpya wa wachezaji.

LALA SALAMA VPL KUENDELEA JUMAPILI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.

Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.

Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.

African Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba.

YANGA, COASTAL UNION ZAINGIZA MIL 66
Mechi namba 172 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Coastal Union iliyochezwa juzi (Mei 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 imeingiza sh. 66,022,000.

Watazamaji 11,478 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,378,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,071,152.54.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 10,230 na kuingiza sh. 51,150,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 69 na kuingiza sh. 1,380,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,819,793.62, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,691,876.17, Kamati ya Ligi sh. 4,691,876.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,345,938.09 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,824,618.51.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)